Katika maadhimisho ya siku ya siku ya uandishi wa Vitabu na Hati Miliki Duniani Afisa Habari wa Kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa (katika ngazi ya Kimataifa) UNIC Bi. Stella Vuzo akizungumza na wanafunzi wa shule mbalimbali waliohudhuria semina fupi iliyoandaliwa na UNIC na kuwafafanulia umuhimu wa kusoma vitabu mbalimbali ambapo wanaweza kujifunza mambo tofauti ikiwemo kujua takwimu za ugonjwa hatari wa Malaria hapa nchini ambao umekuwa ukiongoza kwa kusababisha vifo vya watoto wenye umri chiniya miaka 5, hivyo kwa usomaji vitabu wanaweza kujua namna ya kujikinga na wanapogundua dalili kuweza kuwahi kupata matibabu.
Msaidizi wa Maktaba ya UNIC Harriet Macha akiendesha chemsha bongo kwa wanafunzi walioshiriki semina hiyo kupima uelewa wao kuhusiana na Ugonjwa wa Malaria.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Usomaji na Maendeleo Bi. Demere Kitunga ambaye ni mmiliki wa Book Cafe iliyopo maeneo ya Mikocheni jijini Dar akiwaelezea wanafunzi umuhimu wa kuwa na nia na dhamira ya kujenga utamaduni wa kujisomea vitabu vya nyanja mbali mbali ikiwemo vya Kiada, Ziada na vya maarifa ambapo amewapa changamoto kujianzisha Maktaba binafsi na vikundi ambapo wanaweza kuchangishana fedha kidogo kwa uwezo wao ili kuweza kujinunulia kitabu ambacho wanaweza kushirikiana kusoma ambavyo vitawapa uwezo wa kujitambua, kuwa na maamuzi, kupata uelewa wa vitu tofauti vinavyoweza kuwajengea kujiamini na kuwawezesha kubadilisha mfumo wa maisha katika makuzi yao.
Katibu Mkuu wa Mtandao wa Vilabu vya Umoja wa mataifa Tanzania (UNCTN) Bernadetha Mshana akionyesha moja ya kitabu kilichomsaidia kuweza kupata uelewa wa kuongea Kingereza kwa urahisi zaidi ikiwa ni ushuhuda wake kwa vijana wenzake kuwa usomaji vitabu hupanua uelewa wa mtu na kujua mambo mengi.
Afisa habari wa UNIC katika ngazi ya Taifa Usia Nkhoma akitoa neno la shukrani kwa wanafunzi walioshiriki semina fupi iliyoandaliwa na kitengo cha habari cha Umoja wa Mataifa UNIC katika maadhimisho ya siku ya uandishi wa Vitabu na Hati Miliki Duniani. Siku hii imetengwa rasmi ili kuhamasisha usomaji, auandishi na uchapishaji wa vitabu kupitia hati miliki.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wakisoma vitabu mbalimbali vinavyopatikana katika Maktaba ya Book Cafe yenye mandhari nzuri ya kujisomea ambapo pia panapatikana viytabu vya watu wazima vinavyohusiana na nyanja mbalimbali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...