Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (Katikati), akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es Salaam jana. Zaidi ya watoto 400, wanaosomeshwa chini ya fao la elimu litolewalo na mfuko huo, wanatarajiwa kushiriki kwenye hafla ya kusherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwa fao hilo Jumamosi tarehe 27/04/2013 kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa WAMA, mke wa rais, Mama Salma Kikwete. Wengine pichani ni Meneja wa Michango wa Mfuko huo, ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Operesheni wa mfuko huo , Cosmas Sasi (Kushoto) na Meneja Uhusiano wa mfuko huo, Bi.Lulu Mengele.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio (Katikati), akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa Habari, makao makuu ya Mfuko huo, jijini Dar es Salaam. Mfuko wa Pensheni wa PPF huwalipia ada na mahitaji mengine watoto wa mwanachama aliyefariki baada ya kuchangia miaka 3 au zaidi.
Kwa Mwaka 2012 peke yake Mfuko umewasomesha watoto 1333 katika shule 765 zikiwemo shule 315 za msingi na 450 za sekondari hapa nchini kwa kuwalipia kiasi cha shilingi millioni 682.
watoto zaidi ya 400 wa Dar es salaam, wanaosomeshwa chini ya fao la elimu litolewalo na mfuko huo, wanatarajiwa kushiriki kwenye hafla ya kusherehekea miaka 10 tangu kuanzishwa kwa fao hilo Jumamosi hii kwenye ukumbi mpya wa mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa WAMA, Mke wa Rais, Mheshimiwa Mama Salma Kikwete. Kushoto ni Meneja wa Michango wa Mfuko huo, ambaye pia ni Kaimu Mkurugenzi wa Operesheni wa mfuko huo , Cosmas Sasi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...