Wanafunzi wa shule mbalimbali za sekondari jijini Dar zikiwemo Makongo, Airwing, Mtakuja Beach na Chang'ombe wakiwa Safarini Kulekea katika ziara ya kutembelea Magofu ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara ambayo yapo kwenye orodha ya urithi wa Dunia katika safari ya iliyoandaliwa na Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) wakati wa kumbukumbu ya Biashara ya Utumwa na kuwaenzi waliopoteza maisha katika biashara hiyo iliyokuwa imeshamiri katika maeneo hayo.
Biashara hiyo ya Watumwa ilifanyika kwa miaka 400 na kuhusisha zaidi ya Waafrika milioni 15 na watu wenye asili ya Afrika ambao walikuwa waathirika wa ukatili wa Utumwa na kuendelea kuteseka na madhara yaa biashara ya Utumwa.(Picha na Mo Blog.)
Kiongozi wa msafara huo Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo (wa tatu kushoto) njiani kuelekea Kilwa Kisiwani.
Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo akitoa mwongozo wa ziara kwa wanafunzi baada ya kufika katika bandari ya Kilwa kabla ya kuelekea Kilwa Kisiwani kwa ziara ya mafunzo ya kumbukumbu za biashara ya Utumwa.
Ambapo alisema lengo la ziara hiyo ni kutaka Wanafunzi kujifunza madhara ya biashara ya Utumwa jinsi ilivyofanyika na madhara yake na ili waweze kusaidia katika jitihada za kuitokomeza biashara hiyo ambayo mpaka sasa bado inaendelea kufanyika kimya kimya katika maeneo mbalimbali nchini na kuwataka kuzijua haki zao za kibinadamu na kutogeuzwa bidhaa za kuuzwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa udanganyifu wa kupelekwa kufanya kazi nchini za kigeni.
Mwl. Mwasi wa shule ya Sekondari Chang'ombe (mwenye nyekundu) akiwa ndani ya boti na wanafunzi kuelekea Kilwa Kisiwani.
Wanafunzi wakiwasili Kilwa Kisiwani.
Picha juu na chini' Tour Giude' Dullah akitoa malekezo ya ramani ya sehemu watakazotembelea wanafunzi hao ili kupata ufajamu wa jinsi Historia ya eneo hilo ilivyokuwa hadi kufikia biashara ya Utumwa na majengo yaliyokuwa yakitumika Karne ya 9 baada ya kuzaliwa Kristo.
Wanafunzi wakichukua maelezo muhimu kutoka kwa Mtaalamu wa masuala ya Historia ya Asali ya Kilwa Kiswani na Songo Mnara wakiwa kwenye makaburi waliyozikwa viongozi waliotawala eneo la Kilwa Kisiwani.
'Tour Giude' Dullah akiendelea kutoa ufafanuzi wa maeneo mbalimbali yaliyotumika enzi za biashara ya Utumwa ikiwemo Misikiti, Gereza na Nyumba ya Sultan Hassan Bin Sultan ambaye alikuwa mtawala wa eneo hilo.
Wanafunzi wakielekea kwenye Gereza maarufu lililokuwa likitumiwa na kufunga watumwa.
Muonekano wa Gereza hilo kwa Nje Lango Kuu la kuingia.
Mhifadhi Mambo ya Kale Kilwa Kisiwani Yussuph Bakari Said (mwenye shati la zambarau) akionyesha Kisima kilichokuwa kikitumiwa na wafungwa ndani ya Gereza hilo.
Wanafunzi wakiangalia Kisima kimoja wapo ndani Msikiti wakati huo.
Mmoja ya wananfunzi wa shule hizo walioitembelea maeneo hayo ya kumbukumbu akishangaa Mzinga uliodumu mpaka leo toka Karne ya 9 baada ya kuzaliwa Kristo.
Mafunzo yakiendelea kutolewa kwa wanafunzi hao.
Moja ya Majengo ya Nyumba ya Sultan Hassan Bin Sultan aliyeoa wanawake 77 enzi za utawala wake.
Mhifadhi Mambo ya Kale Kilwa Kisiwani Yussuph Bakari Said katika picha ya kumbukumbu na Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo aliyeambatana na Phillip Musiba pamoja na wanafunzi wa shule mbalimbali za jijini Dar es Salaam katika siku ya kuwakumbuka wahanga wa biashara ya Utumwa.
Wanafunzi wakisindikizwa na Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo (mwenye kitenge) kupanda boti kurudi Bandarini baada ya kuhitimisha ziara yao Kilwa Kiswani.
Afisa Habari wa ngazi ya kimataifa Kitengo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC) Bi. Stella Vuzo aliyeambatana na mfanyakazi mwenzake Phillip Musiba, walimu waliojumuika na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kilwa katika ziara hiyo katika picha ya pamoja.
Angalizo tu kwa hao wamiliki wa sea tax wajitahidi kuwa na life jackets ili tusijepoteza pesa za kamati ya kufuatilia nani alikuwa mzembe.
ReplyDeleteKwa usalama wetu, ni mtazamo wangu tu
Naona mtoa mada una tuchanganya, pale juu umesema ni gereza wa watumwa hapa. Hapa chini umeonyesha kisima kiko ndani ya msikiti. Kwa sababu ukiangalia ukuta unaozunguka hicho kisima ni ule ukuta uliosema ni gereza la watumwa.Kwa uhalisia ni kwamba uliyeweka mada historia huijui vyema ya Tanzania, kasome tena.Hili si kosa lako; kosa liko kwa sisi wenyewe watanzania kutoandika historia yetu kuanzia mwaka wa sifuri hadi angalau mwaka 1950. Utakuta tunaandika historia reference tunachukua kwa Wajerumani au Waingereza.Sisi wenyewe hatujui kitu. Naomba kazi ya kitaalamu ifanyike ili kujua vyema historia yetu kwa faida yetu na vizazi vijavyo.
ReplyDeletelife jaket za nini? Ngoja ajali itokee uone waheshimiwa watakavyo kuja na hoja, tume, kamati,......na kauli kalikali. Sie tumezoea zima moto hayo mengine tuachie wenzetu.
ReplyDeleteNadhani pia watapata fursa ya kuona sinema ya "The Roots"
ReplyDeletenauona udini hivihivi. tusubiri makombora kati ya waislamu na wakristo.
ReplyDelete