Kufuatia ajali ya
kuporomoka kwa jengo la ghorofa 16
lililokuwa linajengwa katikati ya jiji la Dar es Salaam juzi siku ya Ijumaa Kuu tarehe 29 Machi,
2013 mpaka sasa maiti za watu 30
zimepatikana.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, watu 17
waliweza kuokolewa, wanne kati yao bado
wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Wengine walitibiwa na kuruhusiwa.
Kazi ya kufukua eneo la ajali inaendelea na sasa
inakaribia kufikia ukingoni.
.
Inasikitisha sana.Na haya ni "mapenzi ya Mungu" au?Poleni sana kwa familia zilizopotelewa na wapendwa wao.Na wanaotibiwa nawaombea wapone haraka.Juzi hapa blog ya jamii ilitoa picha za maji ya mvua yasiyofahamu mahali pa kwenda maeneo ya Mikocheni TMJ hospital.Haya nayo ni "Hazard" yanaweza kusababisha majengo kuporomoka yakipenya kwenye misingi ya Majengo.
ReplyDeleteDavid V
ufisadi wa wahandisi: kuiba nondo, sementi, dawa, mbao, mirunda, mabati, rangi, n.k. tutafika?
ReplyDeleteHalafu mtwambie mhandisi kahitimu DIT au UD?