Kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Masoko Bodi ya Korosho,Bi Theophina Nyoni,Kaimu Katibu tawala Mkoa wa Lindi,John Likango na mwisho ni Mwenyekiti wa Ilulu Union Killian Kapamba wakiongoza kikao cha Wakulima wa zao la Korosho,Mkoani Lindi.
Wadau mbalimbali wa zao la korosho wakiwemo wenyeviti
wa Halmashauri na Amcos za mkoa wa Lindi wakiwa katika kikao ambacho
kilitoa maadhimio ya kuuzwa kwa korosho kilo Milioni 17 zilizo ghalani
kwa bei yote itakayoletwa na mnunuzi huku Mkulima atoweza kulipwa kama
alivyohaidiwa.
WAKULIMA wa korosho mkoani Lindi wamekubali kuuza korosho zao chini
ya bei ya dira 1200 iliyotangazwa na bodi ya korosho mwanzoni mwa
msimu mwaka huu.
Makubaliano hayo yalifanyika baada ya Kaimu Afisa masoko wa Bodi ya
korosho Tanzania,Bi Theophina Nyoni kutoa maelezo juu ya mwenendo wa
bei ya korosho katika soko la Dunia ambayo inaonyesha kushuka badala
ya kupanda.
Kikao hicho kilichojumuisha wadau mbalimbali wa zao hilo wakiwemo
viongozi wa vyama vya ushirika vya msingi,Wenyeviti wa Halmashauri za
wilaya za, Mkoa wa Lindi na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Lindi Frank
Magali,na kufanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa.
Nyoni alisema serikali iliweka bei dira 1200 kwa kila kilo moja ya
korosho ikitegemea soko la litapanda lakini hivi sasa limekuwa
likishuka siku hadi siku kutoka 2800 kwa kilo moja hadi 2200 kwa
sasa ambayo hawezi kukidhi kumlipa mkulima shs 1200 kutokana na
gharama za uendeshaji pamoja ushuru wa Halmashauri ulio kisheria.
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa chama cha msingi Umoja wilaya
Liwale Hasani Mpako aliwataka viongozi wa Bodi ya korosho Pamoja na
Serikali kutambua kuwa wakulima wa mikoa ya kusini utegemea zao hilo
kuendesha maisha yao hivyo basi kushuka kwa bei hiyo ni kuhatarisha
maisha ya wananchi hao.
Mpako alisema kutoka na hilo ni wajibu wa serikali kulipia hasara
wanayoipata wakulima kwa kuuza korosho zao chini ya bei dira 1200
ambayo ilitangazwa na bodi ya korosho.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi, John Likango ambae
ndie Mwenyekiti wa kikao hicho alisema kuwa kikao cha pamoja kati ya
wakulima, bodi ya korosho na sekretieti ya mkoa pamoja na wadau
wengine kilipitisha maazimio mawili la kwanza wakulima kwa pamoja
wamekubali kuuza korosho zote kilo milioni 17,600 kwa bei yeyote
itakayopatikana kwa makampuni ya ununuzi.
Likango alisema azimio hilo limejitokeza baada ya kuona hali ya soko
la dunia la zao hilo kuwa tete kwa kuyumba mara kwa mara kutoka shs
2800 hadi 2200 kwa sasa.
Hata hivyo kikao hicho ambacho pia kilienda kwa malumbano,Wakulima
waliadhimia kuchangishana ili Tume waliyoiunda kwenda Ikulu kuonana na
Rais Jakaya Kikwete kufuatia kukosa Imani na Bodi hiyo ikiwa pamoja na
kutotekelezwa kwa Maagizo yake aliyoyatoa katika ziara yake Mkoani
Lindi na kukutana na Wadau Wilayani Kilwa mwishoni mwa mwaka jana
Wakati wa kuteremka kwa mfumo wa hela duniani, wanunuzi wa pamba walilalmika kuwa hawataweza kuyalipa mabenki walikokopa mihela.
ReplyDeleteSerikali ilikimbia hima kuyalipa mabenki hayo mamilioni na mamilioni!
Sijui hizo benki zilikuwa za wa-Tanzania au za nchi za nje?
Yaani umma ulipi mabenki ya nje pesa zake na iache kuwalipa wananchi wenyewe?
Acha mabenki yafilisike; ndio uchumi wa ki-bepari huo!