Balozi Mohammed Mzale.

Tafrija ya Muungano, Ijumaa 26 Aprili 2013, Slurpen festlokale, Lakkegata 79B, Oslo. Mgeni wa heshima ni Mheshimiwa Balozi Muhammed Mzale (Balozi wa Tanzania kwenye nchi za Nordic na za Balkans)


Programu ya Ijumaa, 26.Aprili 2013

20:00 Milango inafunguliwa
21:00 Mgeni wa heshima, Mheshimiwa Balozi Muhammed Mzale anaingia.
21:15 Wimbo wa taifa
21:20-21:35 Mwenyekiti wa Chama Cha Watanzania Oslo (CCW Oslo) Dr. Titus Sendeu Tenga kumkaribisha Balozi Mzale.
21:35-21:45 Rais wa TASAO, Hatibu Mgeja kutoa salaam kwa Balozi Mzale na kwa Watanzania na waalikwa.
21:45-22:30 Balozi Mzale kuzungumza na Watanzania.
22:30-23:00 Maswali ya Watanzania kwa Balozi Mzale.
23:00 Mziki hadi 03:00. Chege atakuwa na program ya kughani kwenye muda huo.

Kama kutakuwa na mabadiliko yoyote tutawajulisha

Mohamed Jumanne Waziri Semboja
Wilhelm Færdensvei 2b
0361 Oslo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Watanzania Oslo,

    Udumu Muungano!

    Nimeanza kwa salamu za kheri:

    Kupelekea Maadhimisho ya Muungano alama kubwa ziwe Jembe na Nyundo.

    Zaidi ya kuwa hivyo ni vifaa vya kazi hasa za shambani kwa kukatia magugu, kulimia kung'olea visiki na kuvunja mawe yaliyopo shambani ili mazao yakue kwa amani, lakini akitokea Mdudu kama nyoka ama kipingamizi NYUNDO na JEMBE hugeuka silaha za kujihami (nimetumia alama hizo za vyombo hivyo tena viwe vya CHUMA kwa MIPINI ya CHUMA sio miti wenyewe mtajaza ni kwa nini nitumie alama hizo Wananchi wa kweli mtanielewa tu), hivyo tuudumishe MUUNGANO ili mazao shambani (AMANI na UHURU) yaweze kumea na kukua vyma ili kutoa mavuno bora na endapo pana asiyetaka hili HAKUNA JINSI , ili kumg'oa ADUI tutalazimika kutumia JEMBE na NYUNDO!

    ReplyDelete
  2. Safi sana,naomba niulize hivi kuna group yoyote kwenye facebook au kuna blog au website ambayo inawakutanisha watanzania wote wanaoishi Norway? mi nipo Ă…lesund mbali kidogo na Oslo kwa hiyo sijui chochote kuhusu jumuiya. please let me know

    ReplyDelete
  3. Wewe Mwananchi Mdau wa 2 wasiliana na Ubalozi Oslo kila kitu utapata huko.

    ReplyDelete
  4. kuna website search kwenye google utaipata, watanzania waishio oslo,

    mdau wa tatu acha fix hakuna ubalozi wa tz OSLO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...