Basi la Tayassar likiwa limeacha njia jioni ya leo,lakini hakuna aliyepoteza maisha.
Pichani kama uonavyo ni basi la Tayassar ambalo abiria wake walinusurika kifo baada ya gari hilo kuacha njia kilometa chache kabla ya kufika njia panda Segera,kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo walieleza kuwa basi hilo lilipata pancha ghafla likiwa kwenye mteremko mkali,"lakini kudra za Mwenye Mungu dereva alijitahidi kwa uwezo wake na matokea yake basi hilo likaacha njia na kwenye kuvamia mtaro kama lionekavyo pichani,aidha katika mtafaruku huo hakuna aliyepoteza maisha zaidi wa tu wachache kupata mshtuko tu",alibainisha mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 20, 2013

    Hiki ni kithibitisho kizuri pia kwamba njia zetu ni nyembamba sana kwa kweli. Angali hilo roli na basi yanavyopisha, labda upanuzi kidogo wa njia unaweza pia kupunguza ajali barabarani..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...