Ajali mbaya imetokea asubuhi hii ikihusisha pikipiki na daladala hii ambazo zilikutana uso uso lakini Kwa BAHATI nzuri dereva wa pikipiki Hiyo (mwenye helmet chini) alipona baada ya kuruka kwenye pikipiki na pikipiki kuharibika vibaya baada ya kukanyagwa na gari. Picha kwa hisani ya mwanaharakati mzalendo blog. Ajali za aina hii zimekuwa nyingi mno jijini Dar es salaam na kwengineko kufuatia wimbi kubwa la bodaboda kila mahali na uendesshaji usiofuata sheria
Balaa asubuhi
Askari wa trafiki wakiwa kazini baada ya ajali hiyo, huku dereva wa pikipiki akisubiri pembeni
Dereva wa pikipiki aliyenusurika
Polisi jamii na wasamaria wema wakijaribu kuinasua pikipiki uvungumi mwa daladala
Dereva wa daladala alijitahidi kuhakikisha anaisaga saga hiyo pkpk kwani angeweza kusimama kabla haijafika uvunguni kote huko ! Chuki na roho mbaya vimetawala.
ReplyDeleteAnon wa kwanza ushaambiwa ajali sasa chuki na roho mbaya ya dereva wa dala2 vinatoka wapi; sasa wewe ndo mwenye roho mbaya, roho ya rada ambayo unapakazia watu mazito bila ya kuwa na uhakika wa picha halisi ya ajali.
ReplyDeleteSiku hizi watu wamekuwa wengi lakini binadamu wachache sana
ReplyDeleteHawajatulia hawa madereva wa Boda, mwone huyu jinsi kichwa chake kama akili yake
ReplyDeleteHAPO UTAKUTA DEREVA WA DALADALA NA BODABODA WOTE HAWANA LESENI YAAANI KAZI KWELI KWELI
ReplyDelete