Kaka Michuzi,
Leo wakati nimekwenda Airport OR.Tambo nilitembelea sehemu ya SAP (South Africa Police Office - Lost and Found) nikabahatika kukutana na Pasipoti moja ya kitanzania iliyokuwa hapo kwa muda mrefu tangu 2009 ilipoingia kwenye boda ya Beit Bridge South Africa kupitia Zambia, Zimbabwe, Tanzania.
Mwenye Pasipoti hiyo anajulikana kwa majina matatu Mr. Rashid Said KATETA, Mzaliwa wa Dar Es Salaam, mwenye pasipoti namba AB330886. Kwa bahati mbaya hakuweka details za jamaa zake kwenye nafasi ya dharura. Inawezekana akawa amebana ndani kimnyaa kama wapiganaji wengine hapa.
Nimeambatanisha nakala ya pasipoti hiyo ili uweze kuona kama unaweza kutupa msaada katika hili kwa kuitangaza. Inawezekana kuna mtu anamjua anaweza kunitafuta katika namba +27 82 538 5254 au atuandikie kwenye: info@tanzania.org.za
Nakushukuru kwa ushirikiano wako wa dhati na wa siku zote.
Ndugu yako,
Habibu Awesi Mohamed,
Pretoria,
kny: BALOZI
Jamaa kajilipua halafu nyinyi mnaweka details zake kwenye Blog ya Ulimwengu. Acheni hizo bwana. Si mwaona sehemu aliyoingilia
ReplyDeleteWatu wengine bana yaani wewe u mwema sana au kinaa tu? umeombwa?
ReplyDeletemchawi sio lazima avae hirizi.
ReplyDeleteKujilipua Sauzi?
ReplyDeleteNa njaa yote ile pale pana maisha gani pale kwa Zuma, watu wana shida tupu usalama wenyewe wa kupima watu wanauza Matikiti maji, Machungwa na Ma-apple!
Ohooo,
ReplyDeletekwa Zulu Natal na Mashoka kwa Mapanga ya Wazulu wakicharuka mwenye pasippoti hiyo atakuwa kweli yu-hai kapona?
SIJAONA TATIZO LA HUYU JAMAA KUWEKA TANGAZO LA MTU KUPOTELEWA NA PASSPORT, TATIZO WABONGO WENGI MLIOKO HUKO SOUTH AFRICA SHULE YA KAYUMBA...HATA MIMI NIKIOKOTA PASSPORT NITAJARIBU KUMTAFUTA HUYO ALIYEPOTEZA, KWA WASOMI WANAJUA THAMANI YA PASSPORT ILA KWA WENZANGU NA MIE WANAONA HAINA MAANA HASA YA TANZANIA ILA UKWELI KWA SASA HATA NIPEWE NYEKUNDU YA MAMA SIITAKI YANGU YA KIJANI NA NATIMBA POPOTE KUWAHARIBIA...NYINYI WENYE HIZO ZA RANGI SIJUI BLUE MNA MAISHA GANI?ZAIDI YA KUANGALIA VIBIBI NA KUOSHA VYOMBO.
ReplyDeleteNimewahi kupata kisa cha kweli kuwa kuna Watanzania wanaokuja huku Afrika Kusini kwa njia wazijuazo wenyewe. Wakishafika, wanatupa pasi zao za kusafiria kisha wanaomba ukimbizi au kuishi kwa namna wajuavyo. Yapo matukio mengi ya namna hii. Hivyo, inawezekana kabisa kuwa pasi hiyo imetelekezwa kwa makusudi. Hata hivyo, si jambo baya kutangaza maana inawezekana pia kuwa ilipotea.
ReplyDeleteJambo la kushangaza ni kuwa sielewi kwanini vijana wengi wanakuja huku. Afrika Kusini ya leo haina maisha ya kuwafanya watu wakimbie Tanzania. Maisha ni magumu, hakuna kazi, na usalama ni mdogo mno. Watu wanaofikiria kuja Afrika Kusini watafakari marambili. Hali ni maya huku.
WEWE ULIYEENDA SHULE UTAISHI MILELE HAPA DUNIANI ! USITAKE KUJISHAUA MWENYE ELIMU YA KWELI HAWEZI KUITAMBIA ELIMU YAKE KWENYE BLOGU.ELIMU AU BILA ELIMU PESA NDIO KILA KITU
ReplyDeleteMambo ya kawaida.jamaa alikuwa anajaribu kusaidia lakini sasa anashutumiwa but if u flip da page and see the other side bratha yuko poa kwani what if the dude realy need nondo yake or amekwama kiukweli.
ReplyDelete