Mwenyekiti wa
Chama cha CUF, Mheshimiwa Profesa Ibrahim Lipumba amekaririwa na Gazeti la
Mwananchi la leo, Jumatano, Mei 15, 2013 akisema kuwa “amenasa taarifa za siri za kuwepo kwa mipango ya kuongeza muda wa
Serikali ya sasa kukaa madarakani”.
Katika habari
hiyo iliyoandikwa chini ya kichwa cha habari, “Lipumba: Kuna njama za kumwongezea JK muda” Mheshimiwa Lipumba
anadai kuwa Serikali ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete “ itakaa
madarakani hadi mwaka 2017” kwa
sababu kuna “wasiwasi kuwa mchakato wa
sasa wa kupata Katiba Mpya hautaweza kukamilika mwaka 2014.”
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais, Ikulu, inapenda kufafanua kuwa taarifa hiyo ya Mheshimiwa Prof.
Lipumba ni uzushi mtupu na ni upotoshaji usiokuwa na msingi. Rais Kikwete hafahamu kuwepo mipango
hiyo. Ni vyema Mheshimiwa Lipumba aisaidie
jamii kusema nani anafanya mpango huo ili ukweli ujulikane. Aidha, Mheshimiwa Rais anawasihi wanasiasa na
Watanzania kwa ujumla kuacha tabia za uongo na uzushi na kuwapotezea muda Watanzania
kufikiria mambo yasiyokuwepo.
Ukweli ni
kwamba, kama ambavyo amesema mara nyingi, ni matarajio ya Rais Kikwete kuwa
mchakato wa Katiba utakamilika mwaka 2014 na kuwezesha Uchaguzi Mkuu wa 2015
kufanyika chini ya Katiba Mpya kama inavyotarajiwa na kumpa nafasi ya kustaafu
mwisho wa kipindi chake cha uongozi wa taifa letu.
Imetolewa
na:
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
15
Mei, 2013
Michuzi, since you have direct or close relationship with his excellency interms of news dissemination, kindly advice for 'kurugenzi ya mawasiliano' information dissemination brush up, this kanusho, lile kanusho la dr slaa na matamshi mengi kutoka Ikulu yamekaa kimipasho, yakikosa weledi na kupunguza hadhi ya mheshimiwa Rais wetu, ni vizuri wafanyakazi wa serikali, hususani mahusiano na mawasiliano, wakitoa tamko kwa niaba ya mheshimiwa Rais wajiepushe kutoa matamshi yanayoonyesha chuki na mkanganyiko, au cheap propaganda za kupondana, pengine, Mheshimiwa Rais ampeleke huyu Salva kwa mwandishi wa hotuba za Rais wa Kenya, a 22year old, and a very bright and articulate young girl, pamoja na dominance kubwa sana ya CORD, hadhubutu kujibu kwa kuviponda bali kwa hekima na kuonyesha ukweli ulipo, ni hayo tu, maana wasaidizi wa mheshimiwa wasifanye wananchi wakajenga chuki na taasisi hii muhimu kwa Taifa letu. natumaini ujumbe umekufikia
ReplyDeleteni mimi mpenda maendeleo , mjenga nchi ninayeunga mkoni jitihada za mheshimiwa Rais wetu.
Your message was stellar, well constructed only came short as far as I'm concerned when you said we ni mpenda maendeleo and you r a due supporter of the present, wow, if u like maendeleo you wouldn't support the dude
ReplyDelete