Januari 24, 2005: Ankal akiwa katika benchi la Serengeti Boys katika uwanja wa Barbourfields jijini Bulawayo, Zimbabwe, wakati wa mpambano wa timu hiyo na timu ya Taifa ya Zimbabwe ya wachezaji walio chini ya umri wa miaka 17 chini ya kocha Abdallah 'King' Kibaden (wa pili kulia).
Chini Serengeti Boys wakipiga jalamba kabla ya mchezo huo ambao vijana hao wa Tanzania walishinda kwa bao 1-0 na kufanikiwa kuvuka kuingia fainali ya kombe la Vijana wa Afrika zilizofanyika nchini Gambia.
Bao la ushindi lilifungwa na Nizar Khalfani dakika ya 36 na kuwapa ushindi wa mabao 4-1 kufuatia mechi yao ya awali wiki mbili zilizopita uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam waliyoshinda bao 3-1
ungetutajia majina hata ya wao walio katika benchi manake wengi sasa wamekuwa watu wazima
ReplyDeleteMichuzi nisaidie ni vipi mwanangu ajiunge na hiyo timu kila siku tunafukuzana kwenye viwanja vya mchangani ili arudi kujisomea, yuko darasa la 7 na ana mpira mzuri.
ReplyDeleteAnkali ulikuwa huna kitambi kabisa ha, yani mika 8 tu umekuwa tofauti , atai , kitambi noma bwana
ReplyDelete