Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo akikagua kinywaji aina ya ‘paw paw wine’ na mkononi akiwa ameshika matunda aina ya ‘rozela’ yanayotumika kwa kutengenezea ‘juice’ wakati alilipotembelea kikundi cha Chimbuko kinachoundwa na watu wanaoishi na Virusi vya UKIMWI Mjini Kyela mnamo tarehe 2, Aprili 2013 ili kujua maendeleo yao. Kikundi cha Chimbuko ni moja kati ya vikundi vya kijamii vinanvyonufaika na mradi wa UKIMWI kwa njia ya uwezeshaji Kiuchumi unaoratibiwa na ILO katika maeneo ipitayo njia kuu ya Tanzania – Zambia. (yaani Chalinze, Ilula, Mafinga, Makambako, Kyela na Tunduma).
Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA
Kwa habari na picha zaidi BOFYA HAPA
leo ankali umechemsha ukurasa mzima wa blog ya jamii una habari mbili tu tena sio habari ni mapicha teh teh teh teh
ReplyDeleteWe baba una lako jambo, unasema ankal ana habari mbili tu? una makengeza? Acheni vijiba vya roho, vitawauwa! Nimefungua blog kama kumi za Bongo hadi sasa ni ankal pekee ana-update. Tena si habari za udaku kama unavyotaka wewe. Habari za jamii na maendeleo ambazo huzipati popote pengine. Ankal piga mzigo kaka, achana nao hao. Usikute huyo ana kiblogu kake kimemdodea anataka kutafuta sifa mgongoni kwako. Pole weeee...
ReplyDelete