Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi (kulia) akizungumza wakati wa majadiliano ya wazi ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa, majadiliano yaliyohusu Usalama na Amani Afrika;Changamoto za mapambano dhidi ya ugaidi katika mazingira ya kudumisha amani na usalama. Katika majadiliano hayo yaliyofanyika Jumatatu wiki hii, Umoja wa Mataifa umetahadharisha kwamba Afrika imo hatarini kugeuka kitovu cha mashambulizi makubwa ya kigaidi ikiwa juhudi za ziada hazitafanyika kuyakabili makundi mbalimbali ya kigaidi kama vile Al-Shaabab, Boko Haram na Al-Qauida
Na Mwandishi Maalum
Kama Matukio ya kigaidi
yanayoendelea kutokea Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na katika
Ukanda wa Sahel ya
Magharibi hayatadhibitiwa ,basi
kuna hatari kubwa kwa Afrika kuwa kitovu
cha Ugaidi na Uhalifu wa Kimataifa.
Umoja wa Mataifa, umetoa tahadhari hiyo, siku ya jumatatu wiki hii,
wakati Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa chini ya Urais wa Togo lilipofanya
majadiliano ya wazi kuhusu Usalama na
Amani Afrika; changamoto za mapambano dhidi ya ugaidi katika mazingira ya kudumisha Amani na
usalama.
Ni katika majadiliano hayo,
ambayo pia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alizungumza, ilielezwa wazi kabisa, kwamba, kama hatua madhubuti,
shirikishi na endelevu hazitachukuliwa na Afrika yenyewe na
kwa ushirikiano na
Jumuiya ya Kimataifa na Taasisi
mbalimbali, basi Afrika itageuka kuwa kitovu cha mashambulizi makubwa ya kigaidi.
Makundi ya kigaidi ambayo
yanaelezwa kujijengea himaya
kuanzia Afrika Mashariki hadi Afrika
Magharibi ni pamoja na Al-Shabaab,Al-Qaida, Boko
Haram na Ansar Eddine
Karibu wazungumzaji wote waliochangia majadiliano hayo, akiwamo
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, licha ya kukiri kwamba vitendo vya
kigaidi ni tisho kwa mustakabali wa Afrika na watu wake, lakini pia walieleza
kwamba hakuna sababu yoyote inayoweza kuhalalisha vitendo vya kigaidi.
“ Hakuna sababu yoyote inayoweza
kuhalilisha ugaidi” akasema Balozi Manongi na
kuongeza “ Ugaidi ni tishio kwa
maadili ya ubinadamu na ni tishio
kwa maendeleo na ustawi wa nchi na watu
wake”.
Balozi Manongi, alieleza kwamba
Tanzania bado inakumbuka vema matukio pacha ya kulipuliwa kwa Balozi za Marekani
nchini Tanzania na Kenya mwaka1998. Matukio
ambayo Balozi wa Kudumu wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice naye aliyakumbushia wakati akitoa
mchango wake.
Aidha Balozi Manongi alieleza
kwamba, Tanzania pia katika siku za hivi karibuni imeshuhudia tukio jingine la kigaidi lililotokea Mkoani Arusha.
Akaeleza kwamba ni kutoka
na matukio hayo na hususani hili lililotokea hivi karibuni, Tanzania kupitia
Kiongozi wake Mkuu, Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete, imedhamiria kwa nvugu zake zote kuukabili uovu huo.
Pia alieleza mikakati mbalimbali
ikiwamo ya kupitishwa kwa sheria za sera zinazolenga kudhibiti vitendo vya
ugaidi na fedha haramu.
Wazungumzaji kadhaa pia walitaka kuwapo kwa juhudi za kina
za kudadisi na kushughulikia matatizo
ambayo kwa njia moja ama nyingine yanachangia kuibuka kwa makundi ya kigaidi.
Baadhi ya matatizo hayo ni pamoja na sababu ukosefu wa ajira kwa vijana wengi, umaskini
uliokithiri, kutokuwapo kwa utawala wa sheria, mbinyo wa demokrasia,
machafuko ya mara kwa mara , na ulinzi hafifu
katika mipaka baina ya nchi na nchi.
Uelewa finyu juu ya tafsiri ya ugaidi kwa viongozi wetu utaliingiza taifa matatizoni na kutuongezea umasikini zaidi ya huu tulio nao.Leo hii unaposimama ktk majukwaa makubwa na kuinadi Tanzania kama muhanga wa matukio ya kigaidi ni hatari sana hasa ukizingatia nchi yenyewe ndio kwanza inatambaa huku ikinyosha mkono wa msaada kwa watalii,wawekezaji na wadau mbalimbali wa nje.Ni vyema kufikiri kabla ya kusema na ikibidi uzalendo utawale kwanza.
ReplyDeleteAnony wa kwanza sadata mwanangu. Sio hayo tu uliyoyasema lakini naomba kuongeza kuwa unapokiri kuwa kwako ndiyo uwaja wa fujo, wajanja watakushauri waje kukulinda, ukiwaruhusu tu umekwisha!
ReplyDeleteHawa viongozi wetu wawe makini sana sio kila kitu watachoambiwa na Mataifa esp ya magharibi au na Marekani au hata hiyo so called UN kuwa ndiyo nyimbo za kuimba nchini mwao,wasome kutoka Iraq,Dunia nzima tulielezwa kwamba kuna silaha za maangamizo lazima ishughulikiwe ili dunia iwe salama baada ya maafa yote yasiosemeka wao wenyewe wanasema hakukuwa na silaha walizozitolea mpaka ushahidi UN katika baraza la usalama.Jee wanaweza KU-irreverse hiyo situation ya vita? Mataifa huwa yana intrest zao na sasa ni Afrika.
ReplyDeletei