1.Fomu za maombi ya wagombea
-Fomu za wagombea zitaanza kuuzwa  tarehe 2/5/2013  saa 2 asubuhi na mwisho w a fomu hizo kuuzwa itakuwa tarehe 15/5/2013 saa kumi jioni.
-Fomu hizi zitapatikana BMT, TAVA na kwa Makatibu wote wa vyama vya mikoa,
-Wagombea wa nafasi za Mwenyekiti ,Makamu wenyeviti, Katibu mkuu na Katibu mkuu msaidizi fomu zao  zitauzwa kwa shilingi laki moja na nusu (150,000)
-Wagombea wa nafasi 8  za wajumbe watanunua fomu kwa shilingi laki moja (100,000)
-Mgombea atalipia ada ya fomu ya nafasi anayoitaka EXIM BANK, TANZANIA VOLLEYBALL ASSOCIATION ACC. NO.0301381117.
-Mgombea atapewa Bank slip ambayo ataiwasilisha na kupewa fomu, atayoijaza na baadaye  kuiscan pamoja  na bank slip na kuituma TAVA- E mail tavatanzania@yahoo. Com kabla au tarehe 15/5/2013 saa kumi jioni
-Siku ya Usaili wa wagombea itakuwa tarehe 16/5/2013 kuanzia saa 4 asubuhi Katika hoteli ya Mkonge jijini Tanga.
-Tarehe 17/5/2013 Kuanzia saa 2 asubuhi mpaka saa 12 jioni  wagombea wataendelea na kampeni zao.
  
2.Sifa za wagombea
-Maombi ya mgombea yapitishwe na chama cha  mpira wavu cha mkoa  kilicho mwanachama wa TAVA
-Mgombea awe anaweza kuandika na kuongea kingereza na Kiswahili
-Mgombea wa mara ya kwanza asiwe chini ya umri wa miaka 30 na zaidi ya umri wa miaka 60
-Awe na elimu angalau ya  kidato cha nne.
-Awe ni mtu maarufu katika familia ya mpira wa wavu
-Awe na uwezo wa kutekeleza majukumu na shuguli za TAVA
-Kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu wenyeviti ,Katibu mkuu na katibu mkuu msaidizi mgombea awe amewahi kuwa mjumbe wa bodi ya TAVA angalau kwa kipindi kimoja.
-Mgombea awe na muda wa kutosha kutekeleza majukumu ya TAVA , angalau siku 30 kwa mwaka katika nyakati tofauti.
Mgombea asiwe amewahi kusimamishwa au kufukuzwa na TAVA, Chama cha mkoa , chama chochote kingine cha michezo au shirikisho lolote la mchezo la kimataifa.

3.Mkutano mkuu wa uchaguzi.
 -Tarehe 17/5/2013 saa 12 jioni Wajumbe wa mkutano mkuu kuwasili jijini Tanga
-Tarehe 18/5/2013 saa 3 asubuhi mkutano kufunguliwa rasimi.
-Tarehe 19/5/2013 Wajumbe kuondoka kuelekea makwao.

4. Gharama za mkutano
-TAVA Itagharimia chakula cha mchana kwa wajumbe wote  tarehe 18/5/2013 siku ya mkutano.
 Chama  cha  mkoa kiwalipie wajumbe  wake  malazi, na nauli zao za kwenda na kurudi.

.
Taarifa hii imetolewa na Mwenyekiti wa TAVA.
Augustino Israel AGAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 01, 2013

    Kwanini Taarifa itolewe na Mwenyekiti na sio katibu wa chama? Na kwanini kila uchaguzi ni lazima ufanyikie Tanga tu,? Je Michuzi unaweza kumtafuta John Zambetakia mahala alipo ili tumshawishi agombee uongozi. tutamlipia gharama za fomu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...