Familia ya Bw. Thomas Martin Kiama wa Bongoyo, Oysterbay, Dar es salaam tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwenu ndugu, jamaa, marafiki, wachungaji, madaktari, wauguzi na wote wenye mapenzi mema kwa moyo wa upendo na kujitoa kwa hali na mali katika kipindi chote cha kumuuguza hadi pale Mungu alipoamua kumtwaa Mama yetu kipenzi, Victoria Thomas Kiama tarehe 11.05.2013 na tukampumzisha tarehe 14.05.2013 katika Makaburi ya Kinondoni.
Ni vigumu kumshukuru kila mmoja binafsi, hivyo kwa moyo mkunjufu tunawaomba mpokee shukrani zetu za dhati. Mungu wa Mbinguni awabariki.
Tunamshukuru Mungu kwa muda wote aliotupatia wa kuishi naye hapa duniani. Bwana Mungu alitoa, naye ametwaa, Jina lake libarikiwe milele na milele.
Amina.



Namkumbuka mtu mmoja aitwae John Kiama tulikuwa wote Kill Boys Sec. Je unamhusu?. RIP Mama.
ReplyDelete