Heshima yako Ankal!!
Nimepitia Blog yetu ya Jamii nikapata taarifa kuwa upo Singapore!! Yaani upo karibu kabisa nasi!! Sisi tupo Macau. Ni Watanzania 12 ambao tunafanya kazi hapa katika Casino kubwa sanaaa na show tunayofanya ni kubwa sanaaa!! Jumanne na Jumatano ni Mapumziko!!
Ombi langu nataka uje ututembelee Ankal. Ningependa kujua utaratibu wako niaje? Hata kama si mwezi huu hata kipindi kijacho, maana huwa tunasikia tu viomgozi wetu na wadau kibao wapo China ama Singapore kama hivyo, lakini hatujui jinsi ya kuwasiliana nao!!
Tunatamani Serikali na Watanzania wenzetu wajue jinsi tunavyoitangaza Tanzania yetu Kimataifa hapa MAcau. Maana ni Bahati sana kuwa katika show kubwa kama hii!!
Naandika kwa niaba ya Watanzania wenzangu tunaofanya kazi Macau katika show ya www.thehouseofdancingwater.com iliyopo ndani ya City of Dream Casino, Macau
Nduguyo
Wabogojo
NB: Nakupa zawadi ya ngoma yangu hii uburudike na wadau
Kipaji kipo!
ReplyDeleteNawatakieni kila la kher.
Ila kumbukeni kuwekeza nyumbani maana kazi hizi umri ukienda ,sijui!!!!!!
Wabongo 'kwanza'nakupeni 5 kwa kuionesha tanzania popote tulipo!! hongera washikaji..
ReplyDeletehuyu jamaa kama angeandaliwa mapema angetupatia medali kibao za olimpiki kwenye mambo ya sarakasi
ReplyDelete