Bw.Henry Kileo akiwa na watuhumiwa wenzake wa mashtaka ya Ugaidi yanayowakabili wakati walipofikishwa Mahakama ya Hakimu mkazi mkoani Tabora kwa mara ya kwanza.
Wanachama wengine wa Chadema ambao wanahusishwa katika mashataka hayo ya Kigaidi ambapo imedaiwa kuwa watuhumiwa walifanya makosa hayo ya Ugaidi na kumjeruhi Bw.Mussa Tesha ambaye ni mwanachama wa CCM wakati wa kampeni za uchaguzi wa Ubunge wa jimbo la Igunga mnamo tarehe 9/9/2011 katika msitu wa Hanihani huko wilayani Igunga.
 Ulinzi katika Mahakama hiyo uliimarishwa ipasavyo.
 Henry Kileo akiwa ndani ya gari pamoja na watuhumiwa wenzake wanne wakisubiri kupelekwa Gereza la Mahabusu hadi watakapoletwa tena Mahakamani hapo mnamo tarehe 8/7/2013

Na Josephat Isango wa Tanzania Daima.

KAIMU Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mkoa wa  Dar es Salaam, Henry Kilewo, anashikiliwa  na polisi , akihusishwa na  tukio la kumwagiwa tindikali, Musa Tesha. 

Tesha alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana Septemba 9, mwaka juzi kwenye kampeni ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga, uliomuweka madarakani Dk. Kafumu Dalali.

Akizungumza juzi na Tanzania Daima kabla ya kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi, Kilewo alisema hajui anachoitiwa na kwamba anatekeleza wito wa jeshi hilo kuwa afike ofisini kwao. 

“Sijui ninachoitiwa, nimepigiwa simu naenda kutekeleza wito, nimesha wataarifu mawakili wangu ninaowaamini, kwa kuwa chochote kinaweza kutokea cha msingi Watanzania wapenda mageuzi waniombee kwa Mungu,” alisema Kilewo.

Wakili wa Kilewo, Peter Kibatala, alisema baada ya mteja wake kuhojiwa kwa muda wa saa tano juzi alielezwa kuwa anapelekwa Igunga, mkoani Tabora kuunganishwa na watuhumiwa wengine katika kesi ya kutumia tindikali na kujeruhi.

Kibatala alisema anasikitishwa na hatua ya jeshi hilo kumnyima dhamana mteja wake ilhali kosa wanalomtuhumu linadhaminika na kwamba hayo ni matumizi mabaya ya madaraka kumzuia mtu kwa zaidi ya saa 24 pasipo kumfikisha mahakamani. Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutumia tindikali na kudhuru watu ni pamoja na  Oscar Kaijage wa Shinyanga na Evodius Justinian wa Bukoba.

Evodius Justinian alikamatwa na Jeshi la Polisi mjini Bukoba na kushikiliwa kwa siku kadhaa kabla ya kusafirishwa hadi jijini Dar es Salaam. Kabla ya kusafirishwa na kufikishwa jijini Da r es Salaam, Justinian alieleza kuteswa na kupigwa na askari waliokuwa wakimzuia katika vituo mbalimbali kuanzia mjini Bukoba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2013

    Mbona watuhumiwa wana amani tofauti na waliowakamata

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2013

    Promotion hiyo, anon#1. Ili kuendelea kuwarubuni watu kama nyie!

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2013

    hahhaha Joyce Kiria full TNGP waliomshauri avae high heels apake lipstick ajibebeshe watoto kwa sekunde eti anamlilia mume usaniii, Na wewe kijana wewe Kileo mbona unaharibu maisha yako mapema hivyo? ni mapito tu utapita

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 27, 2013

      Acha chuki binafsi hizo wewe umeoa au umeolewa? Mnapendana? Watu wakipenda na ubaya gani? Ashauriwe kwani yeye hana akili? Jifunze kupenda maendeleo ya wengine na sio kufurahi nguvu na ubabe unaotumika kudhulumu watu na kuwakosea haki. Mnazulia watu magaidi. Mkiletewa boko haram mtawaitaje? Ndugu wawili marekani waliua watu kwenye marathon na bomu lililotengenezwa kwa pressure cooker - hili ni kosa kubwa sana lakini hawakutuhumiwa kua ni magaidi. Magaidi wenu ni wa midomo. Huyo aliyetekwa na kumwagiwa tindikali alikua wapi siku zote anashtaki leo? Ingekua ugaidi si wangemuua ili wapoteze ushahidi? Mara mnasema alimwagiwa tindikali na watu wasiojulikana mara sasa mnatuhumu watu ambao mnasema hawakujulikana. Kama kuteka mtu ni ugaidi na huko kusafirisha watu kutoka mkoa mmoja hadi mwingine chini ya ulinzi mkali, usiku, kuwateswa na bila hata kuitwa mahakamani na kusomewa mashtaka si ni kutumia nguvu na ubabe? Mtu kama anakosa mshitaki anapeleka kesi mahakamani na wahusika wanatumiwa nakala za mashtaka na kuitwa mahakama. Mtu akikataa kwenda mahakamani ndio itolewe ARREST WARRANT akamatwe. Kuonyesha kwamba mnanguvu ya kushukua madaraka mikononi, nyinyi ndio polisi, ndio jaji, ndio prosecutor kila kitu ni nyie - mliona wapi? Siku zenu zitafika tu MUNGU yupo na mtajuta mliyoyatenda kwa kukumoa watu wasio na nguvu, maskini, hawana hata silaha wala madaraka na dola kama nyie. Nasema MUNGU yupo!!!

      Delete
  4. AnonymousJune 27, 2013

    Ivi kummwagia mtu tindikali ni kosa la kigaidi??mie sijui hasa definition ya terrolist ila huwa naichukulia kama vile osama flani nini!!yaani madege makubwa alafu nduki mpaka kwenye mijengo mirefu au labda kuiba taarifa zenye maslahi ya taifa flani kwa njia ya teknolojia ya hali ya juu.Ila huku kwetu sijui hili neno gaidi linatumika vingine??ipo siku tutasikia mtu akiitwa gaidi kwa kumchapa bakora mwenzie au hata kumsukuma.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 27, 2013

    Tugange maendeleo Watanzania. Muda tunao utumia ktk ZeComedeis za rangi kedekede, Nchi inaondoka, tubaki na mshangao! Maendeleo Kimmkakati ndiyo silaha ya ukombozi wetu nyakati hizi!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...