Nahodha wa timu ya Makumbusho United Hamza Mohamed akipokea kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kutoka kwa Ofisa Maendeleo wa TFF Bw. Salum Madadi baada ya kuibamiza timu ya Mtakuja 5-1 katika mchezo wa mwisho wa mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 uliofanyika kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam Juni 25, 2013.
Nahodha wa timu ya Makumbusho United Hamza Mohamed akinyanua juu kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, baada ya kuibamiza timu ya Mtakuja 5-1 katika fainali ya mashindano hayo ngazi ya mkoa iliofanyika kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013.
Wachezaji wa timu ya Makumbusho United wakishangilia baada ya kutwaa kombe la ubingwa wa Airtel Rising Stars, mkoa wa Kinondoni, kwenye uwanja wa Mwanyamala shule ya msingi jijini Dar es Salaam leo Juni 25, 2013. Makumbusho walishinda 5-1 dhidi ya Mtakuja.
Baadhi ya mashabiki wa kishangilia timu zao katika michuano ya Mkoa ya Airtel Rising star 2013
Timu ya Makumbusho United imetawazwa kuwa mabingwa wa Airtel Rising Stars mkoa wa kisoka wa Kinondoni baada ya kuwafunga bila huruma Mtakuja Beach 5-1 katika mchezo wa fainali wa mashindano hayo ya vijana chini ya umri wa miaka 17. Mchezo huo ulifanyika kwenye kiwanja cha shule ya Msingi Mwananyamala jijini Dar es Salaam leo Juni 25 ,2013.
Mabingwa hao wapya wa ARS ngazi ya mkoa walianza michuano hiyo kwa kishindo walipoitandika Sifa United 3-1 katika mchezo wa ufunguzi uliopigwa katika uwanjwa huo huo Jumapili. Katika mchezo wa leo, Makumbusho wamepata magoli kupitia kwa Premji Stephano (dk 12), Ally Amin (dk 35), Rashid Ngone (dk 38 na 71) na Wllie Kalolo (dk 53) wakati Mtakuja walipata goli la kufutia machozi dakika ya 78 kwa njia ya penati iliyopigwa na Steven Munyu.
Jijini Mbeya, timu ya Mbasco ilitoshana nguvu na timu ya Mbosa Jumatatu Juni 24 baada ya kutoka sare ya 3-3 katika mchezo wa vuta nikuvute wa Airtel Rising Stars. Mbasco walipata magoli yao kupitia kwa Jasco Mwaibabe (dk 20 na 50) na Joel Kasimila dakika ya 68. Mchezo huo ulifanyika kwenye kiwanja cha Magereza Mbeya.
Kwa upande wao, Mbosa walipata magoli yao kupitia kwa Michael Mwashilanga (dk 5), Richard Kalinga (dk 49) na Enock Chikaonga (dk 9).
Mjini Morogoro; timu ya Moro kids iliishinda Anglikana 3-0 katika mchezo mwingine wa Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa uliofanyika kwenye uwanja wa shule ya seconday ya Morogoro. Magoli ya Moro kids yaliwekwa kimiani na Abdul Rashid, Robert Nashon na Evans Nashon. Robert na Evans ni mapacha.
Katika mkoa wa kisoka wa Ilalan, Msimamo Youth Academy walipata ushiindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Buguruni Youth Center katika mchezo mgumu iliofanyika kwenye uwanja wa Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. Goli hilo la ushindi lilifungwa dakika za majeruhi na nahodha wa timu hiyo Rajab Mohamed katika dakika ya 89
Mkoa wa kisoka waTemeke ulitarajiwa kuanza mechi zake za Airtel Rising Stars ngazi ya mkoa jana (leo) katika uwanja wa Twalipo na mkoa wa Mwanza vile vile ulitarajia kuanza mechi zake kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana jana (leo).
Programu hii ya Airtel Rising Stars ni ya Afrika nzima likiwa na lengo la kuendeleza na kukuza mpira wa miguu katika bara la Afrika kwa vijana wanaochipukia waweze kupata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao.
Fainali za ARS Taifa vile vile zitatumika kuchagua timu bora za wavulana na wasichana ambao wataiwakilishaTanzania katika mashindano ya kimataifa ambapo nchi mwenyeji wa michuano hiyo itatangazwa mwezi ujao. Wachazeaji wengine watachaguliwa kwenda kwenye kliniki itakayoendeshwa na makocha kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United


Du cheki madirisha ya jengo la shule yaani kiduchu alafu juu, jamani hata hiyo hewa safi haitapatikana kwa uhakika hivyo ubongo nao hautafanya kazi ipasavyo,hivyo kuathiri uwezo na umakini wanafunzi darasani. Majengo ya shule na vitendea kazi vyake mfano dawati,ubao wa kuandikia lazima vipimwe na wataalamu maalum mfano ukubwa wa dirisha,umbali toka dirisha mpaka linapokaa dawati,urefu wa dawati na kikalio chake uwe wenye ulingano usioleta athari kwa mkaaji, ukubwa wa dawati. Haya yote nimeyaona huku kwa wenzetu na yanatiliwa maanani sana kwakua yana athari ktk uelewa wa mwanafunzi darasani.
ReplyDelete
ReplyDeletemichuzi nashukuru angalau kwa kunionyesha kipande kidogo cha majengo ya shule yangu ya msingi mwananyamala 1981-1987 ndugu yangu sijakanyaga shule hii toka 1987 mpaka hii leo nimeiona kwy picha nashukuru angalau nimeona walau ukuta.tulikuwa tunakaa chini kwy vumbi mpk noma asante sana