Salaam Ankal

Kwa kweli wajumbe wa tume ya katiba wameyatendea  haki maoni ya watanzania  juu ya katiba  mpya. Ingawa  sijapata  muda  wa kusoma  kifungu hata kifungu kwa  utulivu, lakini kwa muonekano wa  awali  rasimu ni  nzuri  na itahitaji marekebisho machache  ya kimsingi.  


Rasimu ya  katiba  imependekeza kuwepo kwa  serikali tatu, yaani ya  Muungano, ya Tanzania zanzibar(ambayo ipo kwa sasa) na ya Tanzania Bara( ambayo katika  katiba ya zamani imo ndani ya serikali ya Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania). Kwa  utaratibu wa tume rasimu ya katiba itajadiliwa katika mabaraza mbalimbali yalioundwa katika ngazi tofauti na baadae kwenye  bunge la katiba  na mwishowe itapigiwa kura ya maoni na itakuwa tayari mwaka 2014. Serikali , inataka   katiba hii ianze  kutumika katika uchaguzi wa mwaka 2015.
 
Angalizo langu:
Iwapo  katiba hii  itapita katika mchakato mzima na ikakubalika kwa wananchi kwamba  tuwe na serikali tatu. Serikali  ya Muungano itakuwa na katiba, Serikali ya Tanzania Zanzibar  wanayo katiba yao, Serikaliya  Tanzania bara itakuwa haina katiba yake, hivyo basi  tutabidi  tuanze  mchakato mpya  wa kupata  katiba ya serikali ya Tanzania bara mwaka 2014. Hili linaweza  kuchukua muda mrefu na pengine kuchelewesha au  kuhairisha  uchaguzi wa mwaka  2015.
 
Sijui serikali na wanasiasa wanaliangaliaje  hili.
Wadau wa blog je mna mawazo gani  kuhusu angalizo hili?

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 05, 2013

    Mambo ya muungano yatapunguzwa, yani liwepo la ulinzi tu. Litashughulikia masuala ya vifaa vya ulinzi tu. Raisi wa muungano ndiyo atakuwa na jukumu lake hilo. Ni zito sana. Lakini ukiangalia kwa juu juu utaona ni hakuna kitu.

    Mawaziri wa ulinzi wa tanganyika na zanzibar watahusishwa na raisi wa muungano.

    Jina la muungano ni: Jamhuri ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika (United Republics of Zanzibar and Tanganyika).



    Rasimu ya katiba iliyopo iendelee kuboreshwa kwa ajili ya Tanganyika. Kule Zanzibar nako waboreshe katiba yao kwa kipindi hichi hichi wakati mchakato unaendelea.

    Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Zanzibar na Tanganyika itakuwa na maelezo ya mwanzo hayo na bunge lake, mahakama yake, na wafanyakazi wake.

    Kila la kheri, tutengeneze kitu kizuri kwa vizazi vijavyo. Tutumie akili sana; tusiwe na jaziba.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 05, 2013

    kwanza nikuweke sawa mdau kuwa hakuna serikali itakayoitwa Tanzania Zanzibar what is tanzania zanzibar?

    kunatuwa na serikali ya Tanganyika, serikali ta Zanzibar na serikali ya Muungano wa tanganyika na zanzibar

    lakini nchi itakayopewa jina la tanzania zanzibar?

    jambo la pili labda hujailewa vizuri hiyo RASIMU rasimu imeweka kila kitu wazi kuwa kutakuwa na katiba ya Zanzibar ambayo ipo tokea awali kutakuwa na Katiba ya Tanganyika ambayo ipo tokea awali..

    kuhusu katiba ya Muungano hakutokuwepo na katiba ya muungano badala yake kutakuwepo na SHERIA ya muungano

    Sheria ya muungano wataachiwa wahusika wa mambo ya sheria wao ndio watakaotoa sheria hiyo

    kwa maana wakiweka katiba kwenye muungano ina maana siku yoyote muungano ukiwa na tatizo itabidi katika ya muungano itolewe na ikitolewa ina maana itabidi kupoteza muda upya kwaajili ya kutengeneza katiba mpya

    ili kusikuwepo na usumbufu wa kutafuta katiba mpya mara kwa mara ndio wakaona wasiweke katika kwenye serikali ya muungano waachiwe wana sheria waweke sheria ya muungano na sio katiba

    nafikiri mpaka hapo utakuwa umepata kuelewa japo kidogo kwa ufahamu wangu mimi juu ya hiyo rasimu iliyotolewa.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 05, 2013

    POLE NA KAZI MDAU. MIMI NAKUUNGA MKONO MIA KWA MIA, SUALA LA SERIKALI TATU LIKIPITA, INA MAANA KWAMBA SERIKALI MOJA ITAKOSA KATIBA, YAANI SERIKALI YA TANGANYIKA. KAZI BADO NI MBICHI KABSAA. IN MY OPINION

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 05, 2013

    Wanalijua hilo, na hiyo imewekwa kimkakati kusogeza japo miaka miwili

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 05, 2013

    Ankal, mi naomba nimtoe wasiwasi mdau kwa angalizo lake kwani ukiliangalia swala hili kwa haraka haraka unaweza ukaliona hilo. Lakini kwa ufahamu wangu mdogo nilionao juu ya jambo hili ni kwamba katika hizo serikali 3, inaonekana kwamba uchaguzi tutakaoufanya mwaka 2015 ni uchaguzi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano, hivyo suala la katiba ya Tanzania bara halitaadhiri mchakato wa uchaguzi kwani tutahitaji katiba ya Tanzania bara isimame kwanza ndipo tufanye uchaguzi wa serikali ya Tanzania bara kama ambavyo wamekuwa wakifanya ndg zetu wa Tanzania Zanzibar. Hivyo nionavyo mimi ni kwamba uchaguzi mkuu wa 2015 utaendelea kama kawaida, na baada ya uchaguzi huo tutaanza mchakato wa kupata katiba ya Tanzania bara na ifikapo mwaka 2020 (kutoakana na katiba itakavyosema) basi unapofanyika uchaguzi mkuu wa JMT basi na uchaguzi wa Tanzania Bara na ule wa Tanzania Zanzibar utakapofanyika......ni hayo tu, Asalaam Aleykum

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 05, 2013

    naona wadau mnashindwa kumwelewa aliyetoa mada...

    huwezi kuunda muungano wa nchi mbili au zaidi bila ya kuwa na nchi hizo mbili au zaidi.... kwa maana hiyo tanganyika na zanzibar inabidi ziwepo kwanza kwa utaratibu unaoeleweka ambao ni katiba zao kamili kabla ya kwenda kutengeneza muungano

    huyo anayesema katiba ya tanganyika simwelewi ni ipi anamaanisha

    pia kama mkisema hii rasimu ni kwa ajili ya katiba ya tanganyika...je wanzibar walikua wanafanya nini kwenye hiyo tume

    kwa uelewe wangu hili swala la muungano limewakoroga sana wajumbe wa tume.... theoretical solution ni serikali moja ila realistically ni ngumu....viongozi waliopo wanaogopa tu muungano usiwafie mikononi mwao kwa hiyo wanajaribu kusukuma tu mbele hili tatizo litafutiwe jawabu na awamu zijazo

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 05, 2013

    Karibu Tanganyika!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 05, 2013

    Yote kwa Yote Tuienzi kauli ya Marehemu Baba wa Taifa Mwl JK Nyerere.
    Mtakapojitenga - kwasababu tu ya ujinga/ulevi wa madaraka.... Mkajiita sisi na wao wao!! Hamtabaki salama! Baaada ya hao wao kuondoka nyie mliobakia mtajikuta kuna waflani na waflani na hao si wamoja! Hapo ndiyo mtakumbuka mlimwaga mboga mkabaki na ugali!! Sssa kuula mkavu ndipo itakuwa kimbembe!! Chezea mwalimu weye!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...