Na Ali Issa Maelezo Zanzibar 21/6/2013.
Matumizi mabaya ya
rasilimali isio rejesheka imechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa
mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo imeleta athari kubwa kwa binaadamu na viumbe wengine
ambao wana hitajika kuwepo duniani wakiwa ni miongoni mwa viumbe hai .
Hayo yamesemwa leo huko katika hoteli ya Oceanview nje kidogo
ya mji wa Zanzibar na Miza Suleiman Khamis kutoka idara ya mazingira
zanzibar wakati
alipo kuwa ikitoa mada juu ya mabadiliko ya Tabia ya Nchi yanavyo
athiri ya Nchi , binaadamu na mazingira yake katika mafunzo wanayo
patiwa wandishi wa habari namna ya kuripoti taarifa zinazo husiana na
mabadiliko
hayo hapa Tanzania (CLIMATE CHANGE).
Amesemamabadiliko hayo ni changamoto kubwa kwa viumbe hao ambao
wao ndio wadau wakubwa wanao hitaji kuishi na kupata frusa za utulivu katika maisha
yao ya kilasiku huku. Amseama hali hiyo ni hatari kwa binaadamu kwani hatima yake imeaza kulet amaradhi yasio
kwisha na kuifanya dunia kuwa jangwa na bahari kupanda juu kutu ambacho ni
mtihani mkubwa .
“hali ya joto inapanda na haishuki (tepreture) kaboni
inapanda juu ,maradhi yana ongezeka ,bahari inapandajuu,maporamako ya udongo imechafua
hali ya nchi hii ni hali mbaya ,”alisema Miza Suleiman.
Alisema hali hiyo inatokana na binaadamu kukata miti kwamatumizi ya makaa ,ongezeko la viwanda duniani
,kuchimba mchanga karibu ya maeneo ya fukwe,kuikata mikoko na kilimo
chakuhama hama . Amesema ili hali hiyo iondoke wananchi wawetayari kufuata
maelekezo ya wataalamu kwa kuiresha raslimali hiyo ambayo huchukua muda mrefu kurejesheka
.
Aidha aliwataka wananchi wabadilishe muelekeo ya matumuzi ya
kuni na badalayake watumie majiko ya gesi ili kuona miti inabakia kutoa
hewasafi ambayo anaihitaji binaadamu .
“hali ya joto imeongezeka wanyama wanakufa ,ufugaji
umepungua ,wamasai sikuhiziwamepungua kufugawanyama ,aridhikame ,haliambayo ni hatari kwetu”
aliongezakusema muezeshaji huyo.
Nao wandishi wa habari wakichangia madahizo waliishauri
serikali na wale walio pewa mamlaka juu ya usimamizi suala zima la mabadilikoya
tabia ya nchi kuweka mikakati kwawatu ambao wanaleta uharibifu wa mazingira
kuchukuliwa hatua za kisheria zinazo faa ili kulikomesha suala zima la
uharibifu wa mazingira .
Aidha walisema kuandaliwe mikakati ya usimamizi ambayo
inaendana na sheria za kimataifa ilikuepukana na hali hiyo ya mabadiliko ya
tabia nchi.


Asante sana Mdau Ali Issa kwa Makala hii.
ReplyDeleteHivi Asilia na fedha kipi ni ghali?
Ni wazi kuwa Asilia ndio ghali kwa kuwa unahiribifu wa Mazingira unapotoikea kuirejesha hali ya mwanzo inakuwa sio kitu rahisi, hata kama itarejea itakuwa na mapungufu.
Zaidi ya Sheria WOTE WAWEKEZAJIWA NJE AU WA NDANI WANATAKIWA WALIPE ADA YA MFUKO WA UHIFADHI WA MAZINGIRA KAMA AMBAVYO WAZIRI WA MADINI NA NISHATI Mhe. Prof. MUHONGO ALIVYO ANZISHA UTARATIBU WA ''ENVIRONMENT PROTECTION SOVEREIGN FUND'' KWA MAMAMPUNI YANAYOCHIMBA MADINI NCHINI TANZANIA.
HII ISIISHIE KTK SEKTA YA MADINI BALI IWE NI SERA KWA KILA SEKTA!