Na Ali Issa Maelezo Zanzibar      21/6/2013.

Matumizi mabaya  ya rasilimali isio rejesheka imechangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa mabadiliko ya tabia ya nchi ambayo imeleta  athari kubwa kwa binaadamu na viumbe wengine ambao wana hitajika kuwepo duniani wakiwa ni miongoni mwa viumbe hai .

Hayo yamesemwa leo huko katika hoteli ya Oceanview nje kidogo ya mji wa Zanzibar na Miza Suleiman Khamis  kutoka idara ya mazingira zanzibar wakati alipo kuwa ikitoa mada juu ya mabadiliko ya Tabia ya Nchi yanavyo  athiri ya Nchi , binaadamu na mazingira yake  katika mafunzo wanayo patiwa   wandishi wa habari namna  ya kuripoti taarifa zinazo husiana na mabadiliko hayo hapa Tanzania   (CLIMATE CHANGE).

Amesemamabadiliko hayo ni changamoto kubwa kwa viumbe hao ambao wao ndio wadau wakubwa wanao hitaji kuishi na kupata frusa za utulivu katika maisha yao ya kilasiku huku. Amseama hali hiyo ni hatari kwa binaadamu  kwani hatima yake imeaza kulet amaradhi yasio kwisha na kuifanya dunia kuwa jangwa na bahari kupanda juu kutu ambacho ni mtihani mkubwa  .

“hali ya joto inapanda na haishuki (tepreture) kaboni inapanda juu ,maradhi yana ongezeka ,bahari inapandajuu,maporamako ya udongo imechafua hali ya nchi hii ni hali mbaya ,”alisema Miza Suleiman.

Alisema hali hiyo inatokana na binaadamu  kukata miti kwamatumizi  ya makaa ,ongezeko la viwanda duniani ,kuchimba mchanga karibu ya   maeneo ya fukwe,kuikata mikoko na kilimo chakuhama hama . Amesema ili hali hiyo iondoke wananchi wawetayari kufuata maelekezo ya wataalamu kwa kuiresha raslimali hiyo ambayo huchukua muda mrefu kurejesheka .

Aidha aliwataka wananchi wabadilishe muelekeo ya matumuzi ya kuni na badalayake watumie majiko ya gesi ili kuona miti inabakia kutoa hewasafi ambayo anaihitaji binaadamu .

“hali ya joto imeongezeka wanyama wanakufa ,ufugaji umepungua ,wamasai sikuhiziwamepungua kufugawanyama   ,aridhikame ,haliambayo ni hatari kwetu” aliongezakusema muezeshaji huyo.

Nao wandishi wa habari wakichangia madahizo waliishauri serikali na wale walio pewa mamlaka juu ya usimamizi suala zima la mabadilikoya tabia ya nchi kuweka mikakati kwawatu ambao wanaleta uharibifu wa mazingira kuchukuliwa hatua za kisheria zinazo faa ili kulikomesha suala zima la uharibifu wa mazingira .

Aidha walisema kuandaliwe mikakati ya usimamizi ambayo inaendana na sheria za kimataifa ilikuepukana na hali hiyo ya mabadiliko ya tabia nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 22, 2013

    Asante sana Mdau Ali Issa kwa Makala hii.

    Hivi Asilia na fedha kipi ni ghali?

    Ni wazi kuwa Asilia ndio ghali kwa kuwa unahiribifu wa Mazingira unapotoikea kuirejesha hali ya mwanzo inakuwa sio kitu rahisi, hata kama itarejea itakuwa na mapungufu.

    Zaidi ya Sheria WOTE WAWEKEZAJIWA NJE AU WA NDANI WANATAKIWA WALIPE ADA YA MFUKO WA UHIFADHI WA MAZINGIRA KAMA AMBAVYO WAZIRI WA MADINI NA NISHATI Mhe. Prof. MUHONGO ALIVYO ANZISHA UTARATIBU WA ''ENVIRONMENT PROTECTION SOVEREIGN FUND'' KWA MAMAMPUNI YANAYOCHIMBA MADINI NCHINI TANZANIA.

    HII ISIISHIE KTK SEKTA YA MADINI BALI IWE NI SERA KWA KILA SEKTA!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...