Mahmoud Ahmad,Arusha

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni,Freeman Mbowe na Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini,Godbless Lema wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa ilikuweza kutoa ushahidi wa tukio la bomu lililotokea kwenye mkutano wa kampeni wa chama hicho.

Viongozi hao wanashikiliwa baada ya Mwenyekiti huyo kudai anawajuwa waliolipua bomu na wanao mkanda wa tukio zima la ulipuaji huo wa Bomu kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Udiwani ulikuwa ufanyike Juni 16 jijini hapa.

Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Polisi mkoani hapa jana,Kamishna wa Upelelezi wa Jeshi hilo,Paul Chagonja alisema kuwa jeshi hilo linawataka viongozi hao waweze kuwasilisha ushahidi huo na kuwa kama hawatakubali kwa hiyari basi litawatafuta popote walipo.

Kamishna Chagonja alisema kuwa ushahidi wa tukio hilo ni muhimu kwa amani ya nchi yetu na kuwa machafuko yanayotokea kwenye jiji hili hayakubaliki kwani nchi yeyote iliyoingia kwenye machafuko ilichangiwa na vyombo vya habari kuripoti kwa ushabiki badala ya kutumia taaluma.


“Matukio ya ulipuaji wa mabomu kwenye nchi yetu hayakubaliki na kuwa mtu mwenye ushahidi wa tukio la bomu kwenye mkutano wa chadema atusaidie kuweza kufanya upelelezi wa tukio hili nawaombeni wanahabari kuacha ushabiki na kujikita katika taaluma yenu”alisema Chagonja.


Wakati huo huo Mwili wa aliekuwa Katibu wa Kata ya Sokoni 1 wa Chama hicho,Marehemu Judith William Mushi imepelekwa kuzikwa kwenye kata hiyo kwa heshima zote za chama hicho wakiwemo wabunge mbali mbali wa chama hicho waliopo mkoani hapa baada ya mwenyekiti wao kuwataka kushiriki kwenye tukio hilo.

Baadhi ya wabunge wa chama hicho waliopo mkoani hapa kushiriki msiba huo ni pamoja na mch.Peter Msigwa,Joseph Mbilinyi,Theresia Pareso,Ezekie Wenje,John Mnyika,na viongozi mbali mbali wa chama hicho kutoka makao makuu na mikoa ya jirani.

Aidha baadhi ya wananchi waliongea na mwanahabari hii waliieleza kuwa tumekuwa tukitafuta vipaji vya riadha hapa nchini lakini kumbe wapo hadi wabunge wanaoweza kutuwakilisha vizuri nchi yetu na tukapata hadi medali akiwemo mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema.

“unajua ndugu mwandishi mabomu sio mchezo yalimfanya mbunge kutimua mbio hadi maeneo ya sanawari hapa vipaji vipo ila hatujaweka mkazo kwenye kutafuta vipaji “alisema Yusuph.

Msafara wa kuupeleka mwili wa katibu wa kata ya Sokon 1 ulipitia kwenye barabara za Sokoine kuelekea Esso hadi Pallotkwenye nyumba yake ya milele na kuhudhuriwa na wafuasi wa chama hicho wengi wakitembea kwa miguu umbali wa kilometa sita kutoka Hospital ya mkoa ya Mout Meru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2013

    Kweli utu watu umewatoka hata kwenye misiba wanaleta utani

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2013

    The Psychological Effects of Uniforms.

    Look it up

    ReplyDelete
    Replies
    1. AnonymousJune 20, 2013

      Unajua last year niliona CNN Anderson cooper kwamba kiongozi yoyote anaevaa uniform tuu ni dictator .wakaanza majina ghafafi kuna Wakati nguo za jeshi kutwaa na nyota za kila aina hata Sadam Hussein ,North korea na jacket lake kutwaaaa,Mao wa china na suti Zake ata Nyerere alivaa sana hizo.Fimbo Nyerere fimbo na Mtu Mtu na fimbo .Anderson cooper Kwenye lile discussion waka conclude Politician are narcisstic

      Delete
  3. AnonymousJune 20, 2013

    Angekufa mzaz au mwanae asingeleta mzaa wa haina hiyo,hayo ndiyo madhara ya kuvimbiwa makande .

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 20, 2013

    poleni sana wafiwa. Mungu aiponye tz na watu wake.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2013

    Duh,chadema noma,wafuasi wake wapo kwa ajili ya kutukana,kukejeli viongozi na kutoa sifa zakijinga,sehemu zao kuu ni facebook,jamii forum na arusha..
    The real and lasting victories are those of peace, and not of war.
    Ralph Waldo Emerson

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2013

    Mbona Mbunge wa Kigoma Kabwe Zitto
    Hahuzulii Mazishi Arusha?? Na Vikao vingi haonekani?

    ReplyDelete
  7. Nyie wote hapo juu ni vilaza tu na hamjui mpo dunia gani! wapuuzi kama wazazi wenu

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 21, 2013

    Astaghfir Allah
    Ewe Mnyalu wafikiri watu wote na wazazi wao wapuuzi,yaani hawana akili isipokuwa wewe. Umesema makubwa lakini nafikiri you are using the wrong mouth.Samahani kidhungu sitaki kuwakera waswahili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...