Rais wa Sri Lanka, Mhe. Mahinda Rajapaksa anatarajiwa kuwasili nchini tarehe 27 Juni, 2013 kwa ziara ya kitaifa ya siku mbili.

Siku ya kwanza ya ziara yake, Mhe. Rajapaksa atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete na kushiriki Dhifa ya Kitaifa.

Tarehe 28 Juni 2013, Mhe. Rajapaksa atatembelea Hekalu la Kibudha lililopo Upanga, Jijini Dar es Salaam lililojengwa na Sri Lanka miaka 93 iliyopita.

Aidha, Mhe. Rajapaksa anatarajiwa kushiriki katika Jukwaa la Ushirikiano kwa Manufaa ya Wote (Global 2013 Smart Partnership Dialogue) utakaofanyika kuanzia tarehe 28 Juni hadi 01 Julai 2013. Ataondoka nchini tarehe 29 Juni 2013 kurejea nchini kwake.

IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM

26 JUNI, 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2013

    Ankal huyu haji na watu 700 kama obama?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...