Familia ya Bw. Thomas Martin Kiama, aliyekuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, kwa mara nyingine tena, kwa moyo mkunjufu tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki, wafanyakazi wenzetu na wote wenye mapenzi mema kwa kutufariji kwa hali na mali wakati wa msiba wa mpendwa mama, dada, bibi, rafiki na mke Victoria Thomas Kiama uliotokea tarehe 11 Mei, 2013.
Kwa upendo, tunawaomba wote kujumuika nasi katika Misa ya Shukrani itakayofanyika Jumamosi tarehe 22 Juni, 2013 katika Kanisa Anglikana la Mt. Albano, lilipo karibu na Posta Mpya saa 2 asubuhi, na baadae katika chakula cha mchana nyumbani, Mtaa wa Bongoyo, Oysterbay karibu na Ubalozi wa Kenya.
Tunamuomba Mungu wa Mbinguni aipumzishe roho ya Mpendwa wetu katika amani ya milele.
Amina.
Poleni sana kwa msiba wa mama yetu jamani, nimeshitushwa sana baada ya kusoma tangazo hili. Pole Charles and Ester. Mwenyezi Mungu awape nguvu na uvumilivu katika wakati huu mgumu. Roho ya marehemu ulale mahali pema peponi. Amina.
ReplyDeleteKAGONE MMAAA..
ReplyDeleteHakika ulikuwa zaidi ya Mama kwetu, mshauri, upendo wako kwa ndg na jamaa ni wa kuigwa, umesaidia wengi, tunajivunia kuishi na wewe kwa kipindi ulichokuwa duniani, Tunamuomba Mwenyezi Mungu akupumzishe kwa amani huku tukiyafanya yale mema yote uliyotufundisha na kutuasia. Msiba wako umegusa wengi, Pole kwa Baba Mzee Kiama na wote wenye mapenzi mema na Victoria. R.I.P Mama mdogo TUTAKUKUMBUKA DAIMA
pole Esther Kiama kwa kuondokewa na mama. RIP mama kiama
ReplyDeletePoleni sana, mama Kiama alikua mtu wa watu, mwenye mapenzi mema, pole sana Grace na wengine wote. RIP Mama Kiama - UK
ReplyDelete