Nachukua nafasi hii kutoa shukurani zangu za dhati kutoka katika kilindi cha moyo wangu kwa Hospitali ya Kilutheri ya Hydom iliyoko mkoani Manyara kwa matibabu waliyompatia mwanangu Ally Hassan (16) aliyelazwa hospitalini hapo tokea siku ya Alhamisi Juni 13, 2013 akiwa hajitambui (in a coma) kwa muda wa siku nne mfululizo baada kuugua malaria sugu.

Shukurani maalum ziwaendee madaktari na wauguzi wote wa wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) ambao kwa siku hizo nne tulikesha nao kumuuguza Ally ambaye aliletwa hapo toka Katesh alikoenda kumtembelea mama yake wakati huu wa likizo akiwa hana fahamu. Kwa upendo, weledi na utaalamu wenu hatimaye mlifaniklwa kupambana na malaria hiyo kwa ukamilifu. Hivi sasa Ally hajambo na anaendelea kupata nafuu kila dakika. 

Mama mzazi, Baba mlezi, mjomba, shangazi, mamdogo na mamkubwa mliojitoa kumsaidia Ally nawashukuru sana sana kwa upendo wenu.

 AHSANTENI SANA SANA SANA. 

Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Kilutheri ya Haydom sina cha kuwalipa zaidi ya kutoa ahsante kwa wote mliomshughulikia Ally pamoja na wagonjwa wengine waliolazwa hapo (nilishuhudia kwa macho yangu jinsi mlivyokuwa mkiwashughulikia wagonjwa wote kwa upendo na weledi kila dakika walipohitaji uangalizi) na kupata nafuu. 

Kwa niaba ya wagonjwa wengine waliopata huduma na kupata nafuu, natoa pia ahsante kwa kazi njema, ya weledi na upendo mnaoonesha kwa kila mgonjwa anayefika kutibiwa hapo Hydom. Ninyi ni mfano wa kuigwa katika mahospitali yetu yote hapa nchini. 

NAOMBA MOLA AWALIPE KWA  KUWAZIDISHIA 
PALE MLIPOPUNGUKIWA. MBARIKWE SANA.
AMEN 
-Muhidin Issa Michuzi
Ankal akiwa Haydom na na baba mlezi wa Ally Hassan (kushoto) na mjomba
Sehemu ya mbele ya hospitali ya Kilutheri ya Haydom, Manyara
Baadhi ya wodi za Hospitali ya Kilutheri ya Haydom, Manyara
Ankal akikesha kumuuguza mwanae Ally Hassan hospitalini hapo
Ally Hassan akiwa kitandani pake akiangaliwa na mama, mamdogo, mjomba na shangazi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2013

    Pole saana Uncle kwa kuuguliwa. Tunashukuru kusikia kijana anaendelea kupata afya daily. Kutoa shukrani kwa aliyekufanyia mema ni Utu mwama na hekima. Nami daima nitanzienzi staarabu na hekma kama zako maishani mwangu.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2013

    Pole ankal kwa kuuguliwa. Lakini Mungu ni mkubwa, tunamshukuru kuwa kijana anaendelea vizuri.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 21, 2013

    Hivi huko nyumbani tayari mpo June 30, 2013? Au miye nina makengea?

    Pole Ankali kwa kuuguliwa!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 21, 2013

    Hii hospital ni nzuri sana basi tu ipo huko nje mji..Mungu awabariki sana madaktari wote na wauguzi wanaofanya hapo. Amen
    Mdau Arusha

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 21, 2013

    Where is Manyara, they are already past 30 June 2013. We are still on 21 June 2013 where I live.

    Cheers

    ReplyDelete
  6. AnonymousJune 21, 2013

    Pole sana kaka kwa kuuguza Mola ampe uponyaji wa haraka.Tunawaombea.

    ReplyDelete
  7. poleni sn ila hiyo hospital in watu karimu sana hata mie nilifika kikazi nilipokelewa kama mtu mmoja mkubwa saaana, nadhani mungu amewapa moyo wa pekee. Mungu awabariki sana

    ReplyDelete
  8. AnonymousJune 21, 2013

    Pole kwa kuuguliwa na mwanao

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 21, 2013

    Zimebaki hospitali chache sana zinazojali uhai wa binadamu. Hapa Dar hospitali zenye majina makubwa hazifanyi hivyo...Kama hali ya huyu kijana ilivyokuwa alivyofikishwa hospitali, AAAAA hapa ungekuta manesi wako koridoni wanase: "huyu tunamkunja sasa hivi" bila hata kujitahidi kuokoa maisha

    Nafikiri wadau wenzangu mtaniunga mkono. Nami nikishirikiana na ndugu jamaa wa huyu kijana , naishukuru hospitali hii kwa jitihada walizoonyesha.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 21, 2013

    Pole sana Ankal, ALLAh azidi kumpa afya njema yeye na wagonjwa wengine Allahumma Amin

    ReplyDelete
  11. AnonymousJune 21, 2013

    Mimi kama mdau wa hiyo hospitali ya Hydom kwa kweli nawapa "Hongereni" sana kwa huduma wazifanyazo hasa sifa zimwendee Daktari Mkuu Dr. Olsen na timu nzima. Maadili yao ni ya kuwahudumia wananchi wote bila kujali dini, kabila. Daima hospitali hiyo ya KKKT ina huduma nzuri sana, Mungu awazidishie huruma yenu kwa wagonjwa. Watu wanatoka kila pande za nchi wanatibiwa pale Hongera sana Mkuu wa KKKT: Dr. Alex Malasusa zidisheni huduma hii kwa wagonjwa.

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 21, 2013

    Pole sana kaka Michuzi, Tupo pamaoja katika kumuombea mgonjwa apone haraka.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 21, 2013

    pole sana kwa kuuguza Mungu atakujalia

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 21, 2013

    Katika hali hii, hapa hospitali kuna kitu cha ziada. Maana kwa mtanzania wa leo kutoa huduma nzuri hivi, mie siamini.

    Labda kama kiongozi wa hospilali si mzungu, basi hawa manesi ni wa kuchonga. Vinginevyo ,Mungu awabariki sana

    ReplyDelete
  15. AnonymousJune 21, 2013

    aise ni kweli aliyosema mtu hapo juu, nimeshuhudia kwa macho yangu nilivouguliwa na mtoto wa dada hapa Dar alikua coma siku 6 malaria sugu , hawakuchukua juhudi kabisa manesi na madokta mpaka tukafanya mkakati mkubwa sana na mashinikizo makubwa kupitia sehemu nyeti ndio ikawa salama yake. pole Ankal bora alikua huko

    ReplyDelete
  16. AnonymousJune 22, 2013

    Pole ankal michuzi kwa kuuguza kijana wetu akiwa katika koma.
    Mungu awe naye katika kipindi hiki kigumu cha mauguzi.

    anko mikidadi-denmark

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...