Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Grace Rubambey (katikati) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko huo, Dk Julie Makani, Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque na mmoja wa watu wanoishi na ugonjwa huo, Arafa Salim Said.
Balozi wa Canada nchini, Alexandre Leveque (katikati) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Wengine kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania Dk Julie Makani na Mwenyekiti wa mfuko huo, Grace Rubambey na mmoja wa watu wanoishi na ugonjwa huo, Arafa Salim Said.
Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania, Dk Julie Makani (kushoto) akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya ugonjwa wa Sikoseli Duniani jijini Dar es Salaam leo. Tanzania ni nchi ya nne duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watu wanaougua ugonjwa wa sikoseli.
Meneja wa Benki ya KCB Tawi la Msimbazi, Philipo Pilla (kulia) akizungumza wakati wa maadhjimisho hayo. Benki ya KCB ni mmoja wa wadhamini wa Mfuko wa Sikoseli Tanzania.
Mratibu wa Huduma za Ugonjwa wa sikoseli katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Deogratias Soka (kulia) akizungumza kuhusu hali ya ugonjwa huo katika hospitali hiyo katika maadhimisho hayo. Inakadiriwa kuwa katika ya watoto 8,000 hadi 10,000 kuzaliwa na ugonjwa huo nchini Tanzania kila mwaka.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2013

    Watanzania umefika wakati kuonesha moyo wa kujitolea khassa kwenye taasisi za magonjwa makubwa kama haya ya sikoseli wapo wenzetu wengi ambao wana uwezo mkubwa wa kifedha lakini katika mambo ya kujitolea kuwasaidia wenzao wamekuwa ni wazito mno tujitahidi sanna kutoa nasio kujionyesha hayo hayatotupeleka mbali

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 20, 2013

    Nakubaliana na anonymous... Watanzania tumeishia kufikiria kuwa kujitolea ni kuzungusha bia pia baa sio kwenye maendeleo ya maana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...