Nani alikudanyanya kuwa 'u-machinga" ni biashara za vijana wa kiume pekee, pengine kakosea!!! kina dada wa Ghana kati kati ya barabara wakichangamkia walaji wa bidhaa mbalimbali katika mataa ya Barabara Kuu, Highway, ya kuelekea mji wa Kumasi, jijini Accra.
National ya Ghana- Uwanja wa Kimataifa wa Mpira wa Ghana-Accra, wakati wa wiki sehemu ya maegesho ya magari inatumika vilivyo kuingiza kipato ili kuuweka katika hali safi muda wote. Sio kusubiri "makusanyo" siku ya mechi.
Waharibifu wa miundo mbinu ya Umma wametapakaa kila kona !!! mfuniko wa shimo la maji taka ukiwa umeota mbaya "ibiwa" na kuacha shimo kubwa kati kati ya barabara na kuwapa kazi ya ziada watumiaji picha imepigwa Mitaa ya Kaskazini ya Karneshie jijini Accra.
Kiota cha Movenpick-Ghana, hata Bongo ilikuepo!!
Matangazo ya biashara katika vyombo vya moto, mobile adverts,kwa sasa ndio yameshika kasi yanawafikia watu wengi kwa muda tofauti kama inavyooneka gari ya Kamisheni ya Kupambana na Ugonjwa na Virusi vya UKIMWI nchini Ghana.
Mlimani City ya jijini Accra, lah taswira za majengo yenye maduka makubwa Supermarkets -Shoprite, Game na Mr. Price.
W-store nao wamo katika msafara.Picha zote na Mdau Florence Lawrence.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 26, 2013

    Duu!! Ghana kuko kama Tanzania tu!! Sikuona tafauti!!!! mweee nataka kuona picha za Nigeria sasa jiji la mafuta tuone panafananajee?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 26, 2013

    ZAFANANA.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 26, 2013

    Mimi nipo Accra Ghana, pamaja na kuwa kimandhari kunafanana Ghana wamepombele sana katika miundombinu haswa barabara, mji umepangika na nyumba za makazi zenye ubaro wa hali ya juu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...