Kwa katuni kedekede, tembelea jarida lako la katuni la mtandaoni, 'nathan cartoon magazine' kila Alhamis. Leo lipo angani kupitia chochoro hii,www.nathanmpangala.blogspot. com
Home
Unlabelled
umbea wa nathan mpangala a.k.a kijasti
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Vita Kimaslahi zaidi!
ReplyDeleteNi bora tungepeleka Majeshi Ziwa Nyasa kuikabili Malawi kwenye maslahi na sisi kuliko Kongo.
TZ wewe mtu mzima sasa!
ReplyDeleteKwa nini usinge jaribu kwa kuzaisha 'jiti' refu kupima kina cha maji hayo badala ya kwenda mwenyewe mzima mzima?
Siri ya Vita isiyokwisha kule Mashariki ya Kongo wanaijua Jamhuri ya Rwanda!!!
ReplyDeleteTZ mjanja kweli kweli. Hajajirusha mzimamzima, kashusha miguu wakati mikono kashikilia. Akiona maji yanafika kwenye kitovu na bado hagusi chini atarudi haraka.
ReplyDeleteTZ jinsi alivyotanguliza tumbo mbele hawezi kurudi tena nyuma, kwani alivyoingia hivyo kutoka sio rahisi.
ReplyDeleteKujaribu na maisha ya watoto zetu; mbona msiende wenyewe kutwa anga za burudani tuuuuu!
ReplyDeleteJamani tusiwe wasiopenda AMANI,Rais Jakaya Kikwete kasema ukweli... kuleta amani ndani ya great lakes region, Rwanda na Uganda waanze kwanza kuongea na wapinzani wao FDLR na LRA kama DRC inavyofanya na wapinzani wao M23...Nafkiri Watanzania tuunge mkono wazo hilo la Mtukufu Rais Jakaya Kikwete.
ReplyDeleteKuna wengi sana hawaelewi kwamba Tanzania ndio nchi inayokumbwa na janga hili la wakimbizi kutoka DRC,Burundi,Rwanda na Uganda.
Jiulizeni kwa nini Rwanda na Uganda hawataki kukaa meza moja na wapinzani wao? jibu hizi ni tishio za Udikteta Afrika Mashariki na Kati.Jiulizeni kwa nini Rwanda ina makabila matatu tu(wahutu,Watutsi na Watwa) ila ya sioelewana? Tanzania ni nchi moja barani Afrika inayo heshimika kwa Amani na Demokrasia.Ndugu Anonymous "Vita Kimaslahi Zaidi" tusipendelee kupromoti vita na hatujui madhara yake...Tanzania imeombwa na Umoja wa Mataifa kupeleka majeshi Kongo sawasawa ungeliombwa kupeleka Darfour ao Syria na Afganistan.
Mdau wa 7 umenena,
ReplyDeleteNi muhimu Rwanda kukaa meza moja na FDLR na Congo kukaa meza moja na M-23 huku Uganda kukaa meza moja na ADF!
Mhe. Raisi Kikwete amesema kweli kabisa na pia mwelekeo huo umeshuhudiwa na MAREKANI kufanya mazungumzo na TALIBAN !!! ni kitu ambacho huwezi kuamini Marekani wameona wakae na Taliban huko AFGHNISTANI ili amani irejee na vita isiyokwisha kusimama.
Marekani ilianza kufanya maongezi hayo kwa siri huku Serikali wanayoilinda ya Afghanistani ya Hamid KARZAI ikiwa haijui lakini baadaye wakaja gundua kuwa maongezio kati ya AMERICA na TALIBAN yapo na juzi tu mpango wa AMANI umewekwa wazi.
Sasa kama MAREKANI inaongea na TALIBAN(Magaidi) kusitisha vita na kuleta amani, je ni kosa gani alilofanya Mhe. Raisi Kikwete kumshauri Raisi Paul Kagame na Rwanda kufanya maongezi na FDLR?
Ndio maana baada ya ushauri huo kwa kuwa Raisi Kagame ni mtu makini sana hakujibu kitu, ni kuwa ameridhia ushauri wa Mhe. Raisi Kikwete na kuwa amekubali kuwa ameelezwa ukweli!
Hawa Rwanda nao wana makubwa!
ReplyDeleteOhhh Raisi Jakaya Kikwete na Tanzania yake ametudhalilisha kutushauri tuongee na Waasi wa FDLR!
Dira ni kuleta amani ya kudumu sio mtu kudhalilika ama kudhalilishwa.
Sasa kama Serikali ya Obama ya MAREKANI inaongea na TALIBAN kwa nini Rwanda na Kagame wasiongee na FDLR?