Shirika la Utangazaji la Sauti ya Amerika Idhaa ya Kiswahili (VOA) ikishirikiana na USAID limeandaa mkutano mkubwa wa Vijana utakao fanyika kesho mjini Dodoma maarufu kama Je Nifanyeje?.
 
Washiriki wa mkutano huo ni vijana mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) pamoja na Vijana wengine wa mtaani Dodoma wamealikwa kuhudhuria.

Mtangazaji Mashuhuri  aliyejiunga na idhaa hiyo mwaka 2008 akitokea kituocha ITV na Redio One Sanday Shomari ndiye atakuwa akiongoza mkutano huo.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Habari wa Bunge mjini Dodoma, Sande Shomari pamoja na Bi. Rose Mwakitwange (pichani juu) wamesema maandalizi  ya mkutano huo yamekamilika na mjadala wake utarushwa moja kwa moja na redio Mshirika ABM FM ya mjini Dodoma.

Aidha Bi Rose Mwakitwange ambaye aliwahi kuwa C.E.O wa New Habari Group amewataka wanahabari nchini kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuandishi na wazitumie katika kuelimisha umma na kujipatia kipato zaidi.

Mwakitwange amesema kuwa Wanahabari wana wajibu wa kuisaidia jamii kufahamu vitu vingi vinavyowatatizo hivyo Mwandishi wa Habari akitumia vyema taaluma yake ndiye mtu pekee anaeweza kujibu maswali hayo ya jamii katika nyanja mbalimbali kwa kuandika vitu kwa undani na umakini.

Pia amewataka waanahabari kujitokeza na kujiandikisha ili washiriki Mkutano wa Mafuta na Gesi maana utawawezesha kufahamu masuala mbalimbali na kuwapa mbinu za namna ya kuandika habari zihusuzo gesi na mafuta nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...