Mahakimu Mkoani Lindi wametahadharishwa kutojiwekea malengo makubwa ya
kutaka kujipatia utajiri wa haraka haraka tofauti na vipato vya
mishahara yao ili kujiepusha na uwezekano wa kujitumbukiza kwenye
vitendo viovu vya kuomba rushwa na hivyo kupindisha maamuzi ya utoaji
haki kwa jamii ikiwemo wanyonge kutokuwa na haki.
Taadhari hiyo imetolewa na katibu msaidizi idara ya viongozi wa
utumishi wa umma/siasa Bi Zahara Guga kwenye mafunzo ya kuwaaelimisha
mahakimu Mkoani humo juu ya kusimamia utoaji wa haki kwa kufuata
sheria, kanuni na taratibu ili kuwatendea haki wananchi.
Aidha Bi Zahara Ameonya kuwa kama utoaji haki kwa wananchi usipofanywa
kwa umakini na uadilifu mkubwa, kuna hatari kwa mahakimu hao wakawa
chanzo cha kulisababishia taifa kuingia kwenye migogoro na hatimaye
uvunjifu wa amani usio wa lazima.
Akifungua Mafunzo hayo,Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Lindi,Joh
Likango alitaja baadhi ya mapungufu na matatizo ya kimaadili kwa
Mahakimu ni pamoja na rushwa , utoaji wa huduma usioridhisha, matumizi
mabaya ya madaraka, wizi, unyanyasaji wa kijinsia pamoja na rushwa ya
ngono.
Likango alisisitiza kuwa Rushwa Imekuwa kero kubwa kwa jamii kutokana
na kukithiri kwenye sekta za umma jambo ambalo linawafanya wananchi
kununua haki zao na kusababisha huduma nyingi za kijamii kutolewa
chini ya kiwango.
‘mahakama ni chombo ambacho kinatoa haki kwa jamii bila ya
upendeleo hivyo basi idara hiyo inawajibu kutekeleza majukumu yake
kuhudumia wananchi bila ya upendeleo ili Haki itolewe bila Chochote
chenye kushawishi vinginevyo Mtapoteza Amani iliyopo”Alimalizia
Likango.
Kwa upande wake Hakimu Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi
Dunstan Ndunguru kwa niaba ya wenzake amewataka mahakimu wenzake
kuyatumia mafunzo hayo kurekebisha kasoro zao ili kuhakikisha kuwa
wananchi wanapata haki wanayostahili pale wanapohitaji msaada wa
kisheria.
Jengo la Mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi Lindi
Kaimu katibu Tawala Mkoa wa Lindi akifungua mafunzo
kwa mahakimu wa mkoa wa Lindi kuhusiana na Maadili.
Mahakimu toka mahakama za mkoa wa Lindi wakiwa katika
mafunzo ya siku moja yaliyotolewa na Sekriterieti ya maadili ya Umma
na kufanyika katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Lindi,John Likango,wa pili
toka kushoto waliosimama akiwa katika Picha ya Pamoja na mahakimu wa
mahakama za mkoa wa Lindi wakiwemo maafisa toka Sekriterieti ya
maadili ya Umma.Picha na Habari zimeleta na Abdulaziz Video,Globu ya Jamii-Lindi.


Tumeshiba! Na watu wetu wamekondeana.
ReplyDelete