Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Lowassa akizungumza wakati wa majadilino yaliyohusu namna ya kuingiza suala la wazee katika ajenda mpya za Maendeleo baada ya mwaka 2015. Mkutano huo ulioambatana na chakula cha mchana ulifanyika siku ya Jumatano hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa na ulioandaliwa na United Nations Foundation kwa kushirikiana na Mashirika mengine ya Kimataifa. katika mchango wake, Mhe. Lowassa amesisitiza umuhimu wa ubia kati ya serikali na sekta binafsi katika kuzikabili changamoto za ongezeko la idadi ya wazee duniani. Inasemekana miaka michache ijayo idadi ya wazee duniani itazidi idadi ya watoto wadogo chini ya miaka mitano. Pamoja na Mhe. Lowassa wengine waliochangia majadiliano hayo ni Bi. Ann Pawliczko kutoka UNFPA wa pili kutoka kushoto, Bw. Jack T. Watters kutoka Pfizer, Bw. Paul Ong HelpAge International, Bw. Sharig Khoja kutoka United Nations Foundation, aliyeketi karibu na Mhe. Lowassa ni Bi. Jane Barratt aliyeratibu majadiliano hayo.
Mhe. Lowassa akipeana mkono na mmoja wa waandaji wa majadiliano hayo kuhusu Wazee, takwimu kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu ( UNFPA) zinazonyesha kwamba mwaka 1950 idadi ya wazee duniani waliokuwa na miaka 60 au kuzidi ilikuwa milioni 205, 2012 idadi hiyo iliongezeka hadi kufikia 810 milioni. Inakadiriwa kwamba idadi hiyo itaongezeka hadi kufikia Bilioni 1 si zaidi ya miaka kumi ijayo na ifikapo mwaka 2050 idadi ya wazee wenye umri wa miaka 60 na kuendelea itafikia bilioni 2. Aidha duniani kote wanawake ndio wanaokadiriwa kuishi umri mrefu zaidi kuliko wanaume.
Sehemu ya washiriki wa majadiliano hayo wakiwamo pia Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao katika Umoja wa Mataifa.
Mhe. Edward Lowassa akibadilishana mawazo na Balozi wa Zimbabwe katika Umoja wa Mataifa, Bw. Chitsaka Chipaziwa.
Mh. Lowasa akiwa na mmoja wa washiriki wa majadiliano kuhusu mstakabali wa wazee.
Dunia zipo tatu, kuna dunia ya kwanza, ya pili na ya tatu.Ongezeko la wazee ktk dunia ipi?bila shaka itakua ni ktk dunia ya kwanza kule ambapo kwenye mifumo mizuri ya maisha,matibabu na huduma za kijamii ikienda sambamba na urefu wa muda wa kuishi.Kwa dunia ya tatu sidhani, mfano huko bongo wala haitaji kufanya uchunguzi haya mapicha tuyaonayo humu bloguni ktk sherehe mbalimbali yatosha kusema kwamba idadi ya vijana ni kubwa kuliko wazee na itazidi wazee hata siku za mbele mpaka pale mifumo yetu itakapo badirika na kua ktk ubora wa kurefusha umri wa kuishi.
ReplyDeleteKwa nchi ya dunia ya tatu kama TZ sikubaliani na kauli yao.
Jamani urefu wa maisha yetu ni miaka 45-55. Population kubwa ni vijana, watu hawaishi kuwa wazee afrika. Ongezeko kubwa na tishio ni vijana ambao hawana ajira huku wakiwa wamesoma.
ReplyDelete