Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani mama Lily Munanka (kati) akiwakaribisha Masanja na Shilole wakiwa pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa kiswahili Marekani, Bwn. Baraka Daudi (kushoto) na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ya maandalizi Bwn. Idd Sandaly Ubalozini hapo Jumanne July 2, 2013 walipokwenda kumtembelea na kufanya kikao kwa kumuelezea Kaimu Balozi maandalizi ya sherehe hii itakayofanyika Jumamosi July 6, 2013 yalikofikia.
Masanja akitia saini kitabu cha wageni Ubalozini hapo.
Shilole akitia saini kitabu cha wageni Ubalozini hapo.
Kutoka kushoto ni Baraka Daudi, Kaimu Balozi mama Lily Munanka, Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Idd Sandaly, Shilole na Masanja Mkandamizaji wakiongea jambo walipokua Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington, DC.
Masanja na Shilole katika picha ya pamoja na Afisa Habari wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga.
Kamati ya Maandalizi wakitoa taarifa kwa Kaimu Balozi mama Lily Munanka maandalizi yalikofikia.
Nyammy katika picha ya pamoja na Shilole na Masanja.
Shilole na Masanja katika picha ya pamoja na Mariam.
Mama Love Maganga akipiga picha ya pamoja na Masanja na Shilole.
Shilole na Masanja walipotembelea ofisi za Community Mult Services, Inc zilizopo Silver Spring, Maryland.
Kutoka kushoto ni Mr. Watson, Ms Patricia, Jamila, Shira, Mrs Reese, Shilole, Masanja na Baraka katika picha ya pamoja.
Masanja na shilole wakipata Dinner ya mchana kwenye mgahawa wa Kijiji cha Swahili.
 Mussa Shedafa katika picha ya pamoja na wasanii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 03, 2013

    Jamani hebu tuonesheni hasa kile mlichosema wameenda kufanya, naona mnatoa picha za mizunguko tu.. hawa jamaa walienda kufanya jambo gani? na limefanyika? mafanikio? nini wamejifunza ambacho wataleta huku nyumbani kuwasaidia wenzao?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 03, 2013

    Mimi najua masanja atakuwa ameelimika na kuwa muungwana aache kuita wasichana na dada zetu, mama zetu 'viburudisho'. Hayo ni matusi na udhalilishaji (ulaya utafungwa). Mimi najua ni sababu ya kukosa elimu na maadili mema ambalo ni tatizo sana kwa jamii yetu ya sasa.

    ReplyDelete
  3. Shilole unatia aibu unakwenda ubalozi na skintait badilikeni wasanii kila vazi lina sehemu yake

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 03, 2013

    Kusafisha matongotongo Ughaibuni ni jambo muhimu na ya wezekana hilo ndilo wameenda kufanya.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 03, 2013

    Michuzi acha kutuchekesha, what is dinner ya mchana?

    Nawapa big-up wasanii wetu, nawapenda sana

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 03, 2013

    Picha ya kwanza ina maelezo yote shughuli tarehe 6july husomi unaangalia picha tu.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 03, 2013

    Lunch ya mchana? lunch=chakula. Kiswahili oyeeeeeeeee

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 03, 2013

    huyo shilole sijui ndio mavazi gani hayo ya kwenda kwa balozi? wanatutia aibu tu kaenda fanya nini? hebu watu muwa makini jamani kaaa

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 03, 2013

    Dinner ya mchana ndio kitu gani?

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 03, 2013

    Vazi hilo sio la kuzungukia maofisoni. Utadhani anaenda kuimba ubalozini. Dress more decent ukienda sehemu za wadhifa.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 03, 2013

    Mie bado sijaelewa hasa dhima ya ziara hii????hawa ni watu gani kwa huko Tanzania??yaani wanajishughurisha na nini kikubwa kwa manufaa ya Tz na watu wake??

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 03, 2013

    Umafia tu hakuna lolote.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 03, 2013

    Huyo Shilole alikosa nguo yoyote ya heshima ya kuingilia hapo ubalozini,hadi aache makwapa yake nje?!

    ReplyDelete
  14. Wameenda kupiga picha.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 04, 2013

    1. Asubuhi: Watu hupata Break fast au kifunguwa kinywa.
    2. Mchana: Lunch au chakula cha mchana.
    3. Jioni: Dinner au chakula cha jioni/usiku mchanga.

    4. Kama mtu alichelewa kupata break fast asubuhi anaweza kula chakula karibu na mchana yaani kifunguwa kinywa pamoja na chakula cha mchana kwa pamoja, hicho mashetani wanaita brunch. ( yaani late breckfast and early lunch.
    5. Supper. Chakula chepesi cha usiku kinacholiwa saa zimekwenda. Hapa tilia maanani kwamba simaanishi kile ambacho mmoja wa walaji mara nyingine hulia. Ha! ha! ha! ha! haaa!!

    Haya Ankal.

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 04, 2013

    Mwacheni huyo ndiye Shilole ft na Masanjas, akiwa huko uzunguni mwiteni Masanjas, si munajuwa tena.

    Hata nyinyi munaowalaumu mulipofika huko kwa mara ya kwanza mulikuwa kama wao na inawezekana mulikuwa katika hali ya kusikitisha kuliko wao. Tulizeni ngoma, na subilini siku wakirudi huko kwa mara ya pili. Hata yule mgeni wetu, mkuu wa dunia kaomba radhi kasema akirudi tena atapanda gari la wazi ili wananzi wamuone. MAISHA NI KUJIFUNZA TOKANA NA MAKOSA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...