Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Marekani mama Lily Munanka (kati) akiwakaribisha Masanja na Shilole wakiwa pamoja na Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya sherehe ya miaka 3 ya Vijimambo na tamasha la utamaduni wa kiswahili Marekani, Bwn. Baraka Daudi (kushoto) na Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo ya maandalizi Bwn. Idd Sandaly Ubalozini hapo Jumanne July 2, 2013 walipokwenda kumtembelea na kufanya kikao kwa kumuelezea Kaimu Balozi maandalizi ya sherehe hii itakayofanyika Jumamosi July 6, 2013 yalikofikia.
Masanja akitia saini kitabu cha wageni Ubalozini hapo.
Shilole akitia saini kitabu cha wageni Ubalozini hapo.
Kutoka kushoto ni Baraka Daudi, Kaimu Balozi mama Lily Munanka, Rais wa Jumuiya ya Watanzania DMV, Bwn. Idd Sandaly, Shilole na Masanja Mkandamizaji wakiongea jambo walipokua Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani uliopo Washington, DC.
Masanja na Shilole katika picha ya pamoja na Afisa Habari wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani, Mindi Kasiga.
Kamati ya Maandalizi wakitoa taarifa kwa Kaimu Balozi mama Lily Munanka maandalizi yalikofikia.
Nyammy katika picha ya pamoja na Shilole na Masanja.
Shilole na Masanja katika picha ya pamoja na Mariam.
Mama Love Maganga akipiga picha ya pamoja na Masanja na Shilole.
Shilole na Masanja walipotembelea ofisi za Community Mult Services, Inc zilizopo Silver Spring, Maryland.
Kutoka kushoto ni Mr. Watson, Ms Patricia, Jamila, Shira, Mrs Reese, Shilole, Masanja na Baraka katika picha ya pamoja.
Masanja na shilole wakipata Dinner ya mchana kwenye mgahawa wa Kijiji cha Swahili.
Mussa Shedafa katika picha ya pamoja na wasanii


Jamani hebu tuonesheni hasa kile mlichosema wameenda kufanya, naona mnatoa picha za mizunguko tu.. hawa jamaa walienda kufanya jambo gani? na limefanyika? mafanikio? nini wamejifunza ambacho wataleta huku nyumbani kuwasaidia wenzao?
ReplyDeleteMimi najua masanja atakuwa ameelimika na kuwa muungwana aache kuita wasichana na dada zetu, mama zetu 'viburudisho'. Hayo ni matusi na udhalilishaji (ulaya utafungwa). Mimi najua ni sababu ya kukosa elimu na maadili mema ambalo ni tatizo sana kwa jamii yetu ya sasa.
ReplyDeleteShilole unatia aibu unakwenda ubalozi na skintait badilikeni wasanii kila vazi lina sehemu yake
ReplyDeleteKusafisha matongotongo Ughaibuni ni jambo muhimu na ya wezekana hilo ndilo wameenda kufanya.
ReplyDeleteMichuzi acha kutuchekesha, what is dinner ya mchana?
ReplyDeleteNawapa big-up wasanii wetu, nawapenda sana
Picha ya kwanza ina maelezo yote shughuli tarehe 6july husomi unaangalia picha tu.
ReplyDeleteLunch ya mchana? lunch=chakula. Kiswahili oyeeeeeeeee
ReplyDeletehuyo shilole sijui ndio mavazi gani hayo ya kwenda kwa balozi? wanatutia aibu tu kaenda fanya nini? hebu watu muwa makini jamani kaaa
ReplyDeleteDinner ya mchana ndio kitu gani?
ReplyDeleteVazi hilo sio la kuzungukia maofisoni. Utadhani anaenda kuimba ubalozini. Dress more decent ukienda sehemu za wadhifa.
ReplyDeleteMie bado sijaelewa hasa dhima ya ziara hii????hawa ni watu gani kwa huko Tanzania??yaani wanajishughurisha na nini kikubwa kwa manufaa ya Tz na watu wake??
ReplyDeleteUmafia tu hakuna lolote.
ReplyDeleteHuyo Shilole alikosa nguo yoyote ya heshima ya kuingilia hapo ubalozini,hadi aache makwapa yake nje?!
ReplyDeleteWameenda kupiga picha.
ReplyDelete1. Asubuhi: Watu hupata Break fast au kifunguwa kinywa.
ReplyDelete2. Mchana: Lunch au chakula cha mchana.
3. Jioni: Dinner au chakula cha jioni/usiku mchanga.
4. Kama mtu alichelewa kupata break fast asubuhi anaweza kula chakula karibu na mchana yaani kifunguwa kinywa pamoja na chakula cha mchana kwa pamoja, hicho mashetani wanaita brunch. ( yaani late breckfast and early lunch.
5. Supper. Chakula chepesi cha usiku kinacholiwa saa zimekwenda. Hapa tilia maanani kwamba simaanishi kile ambacho mmoja wa walaji mara nyingine hulia. Ha! ha! ha! ha! haaa!!
Haya Ankal.
Mwacheni huyo ndiye Shilole ft na Masanjas, akiwa huko uzunguni mwiteni Masanjas, si munajuwa tena.
ReplyDeleteHata nyinyi munaowalaumu mulipofika huko kwa mara ya kwanza mulikuwa kama wao na inawezekana mulikuwa katika hali ya kusikitisha kuliko wao. Tulizeni ngoma, na subilini siku wakirudi huko kwa mara ya pili. Hata yule mgeni wetu, mkuu wa dunia kaomba radhi kasema akirudi tena atapanda gari la wazi ili wananzi wamuone. MAISHA NI KUJIFUNZA TOKANA NA MAKOSA.