Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
amemhamisha Engineer Ibrahim Iyombe,
aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwenda
kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi.
Taarifa
iliyotolewa Dar es Salaam leo, Alhamisi, Agosti 22, 2013 na Katibu Mkuu
Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue imesema kuwa Eng.
Iyombe anachukua nafasi ya Engineer
John Stanslaus Ndunguru ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Aidha,
taarifa imesema kuwa uhamisho huo unaanza mara moja.
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
Hongera sana Eng.Iyombe tunafahamu we ni jembe letu,mutu wa watu nenda ukafanye yako pale ujenzi!
ReplyDeleteIyombe ni jembe c mchezo.all the best
ReplyDelete