Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja (pichani) ameelezea furaha na shangwe yake kufuatia ushindi wa jana, Jumatano Agosti 07, 2013 kwa Jeshi la Magereza kuibuka Mshindi wa jumla katika Maonesho ya Wakulima - Nane Nane Kitaifa yaliyofanyika katika Uwanja wa Nzuguni, Dodoma.

Katika salaam zake za pongezi Kamishna Jenerali Minja pia amewapongeza Wakuu wa Magereza Mikoa, Wakuu wa Magereza yote Tanzania Bara, na Askari wote kwa jumla kwa namna walivyoweza kushiriki kikamilifu katika kuleta ushindi wa kwanza katika Taasisi za Uzalishaji za Serikali, Banda Bora, Kilimo na Mifugo hata katika Maonesho ya Kikanda ikiwemo Kanda ya Magharibi iliyojumuisha Mikoa ya Katavi, Kigoma na Tabora pamoja na Kanda ya Mashariki iliyojumuisha Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro kwa kuibuka mshindi wa kwanza kwa upande wa Taasisi za Uzalishaji za Serikali.
"Nimepokea kwa furaha kubwa na shangwe habari za ushindi huo wa kwanza wa jumla katika Maonesho ya Wakulima Kitaifa na hata ushindi wa kwanza kwa upande wa Taasisi za Uzalishaji za Serikali katika Baadhi ya Kanda ambazo Jeshi la Magereza limeshiriki".
Kwa niaba ya Serikali na kwa niaba yangu mwenyewe, napenda kuwatumia salaam hizo za pongezi kwa ushindi huo kwani matokeo haya siyo yamenyesha tu kama mvua ya ghafla, bali ni matokeo makubwa ya mpango mkakati tuliouasisi - ninyi na mimi tangu nilipoteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kuapishwa rasmi tarehe 25 Septemba, 2012 kuwa Kamishna Jenerali wa Magereza nchini.
Aidha, amesisitiza kuwa ushindi huo bado ni changamoto kwa Jeshi la Magereza kuhakikisha kuwa wanajipanga vyema katika Maonesho mengine yanayofuata ili kuendelea kutetea nafasi hiyo ambayo imeleta sifa kubwa kwa Jeshi la Magereza hivyo kutekeleza mpango kazi wa sasa katika utendaji wa kazi unaotaka Matokeo makubwa sasa(Big Results Now).
Maonesho hayo ya Wakulima hufanyika kila Mwaka Kitaifa na Kikanda ambapo Kitaifa katika Uwanja wa Nzuguni, Dodoma jumla ya washiriki zaidi ya 400 kutoka Wizara, Idara, Taasisi za Serikali zinazojitegemea na Makampuni Binafsi wameshiriki kikamilifu katika Maonesho hayo ambayo yamefungwa jana na Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Seif Idd.
                            Imetolewa na Mkaguzi wa Magereza, Lucas Mboje,
                            Afisa Habari wa Jeshi la Magereza Nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...