Magari ya wagonjwa yalitolewa na Korea Kusini kwa ajili ya majimbo ya vituo vya afya vinne vya majimbo ya Ruangwa na Nchinga Mkoani Lindi.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akionyesha funguo ya moja ya magari ya msaada mara baada ya kukabidhiwa rasmi na Balozi wa Korea Kusini nchini Tanzania, Mhe. Chung IL.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akipungia mkono watu waliohudhuria hafla ya makabidhiano huku akiendesha moja ya magari ya msaada kutoka Korea Kusini. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa pili kutoka kushoto akimpa funguo Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Serikali za Mitaa na Tawala za Mikoa), Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) ambaye jimbo lake la Ruangwa limepatiwa magari mawili.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. shukrani kwa viongozi wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa kweli ukanda wa kusini
    ulisahauliwa miaka mingi kina mama wajawazito wengi walikuwa wana shida ya usafiri mara nyingi huzalia katika mazingara ya shida njiani kwa huduma za usafiri wa shida au majumbani kukosa kabisa huduma. Hongera kwa wabunge kuwepo na mpangilio mzuri wa matumizi ya haya magari yasigeuzwe daladala bubu kwa madereva wasio n nidhamu.
    Mikidadi-Denmark

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...