BIBI Siti Hamad Khamis (pichani) anasumbuliwa na ugonjwa wa figo ambazo zimeshindwa kufanyakazi. Kwa hiyo anaomba msaada kutoka kwa wasamaria wema utakaomuwezesha kutibiwa.
Amelazimika kuomba msaada wa hali na mali ili kuokoa maisha yake kutokana na gharama kubwa za matibabu zinazoendelea kuikabili familia yake kwa muda mrefu sasa. Kwa mfano kila wiki anatakiwa kwenda hospitali mara tatu ambapo kwa siku hulipa sh. 350,000.
Matibabu anayopatiwa ni kusafishwa damu ili kupunguza sumu mwilini, kupimwa na chanjo.
Anaomba kwa wale watakaoguswa na tatizo linalomsumbua, wamsaidie matibabu ndani na nje ya nchi au wamchangie kupitia AC 2011601674 Benki ya NMB, tawi la Bank House.
Au wawasiliane na mumewe kwa simu namba 0774215217.
Ahsanteni.
nimejaribu kumpigia huyo bwana kwenye hiyo namba lakini simu haipatikani; nilitaka kumshauri kwamba kwa hii hali ilipofikia ni vizuri kupata ushauri wa kitaalam kuona uwezekano wa kubadilisha figo za huyu mama; suala kubwa ni donor ambae atakuwa tayari kumpatia figo moja huyu mgonjwa; hili moja kwa moja lianze na wanandugu; ajitokeze mmoja ambae atakuwa tayari kumpa mgonjwa figo (once ikugundulika kuwa inafaa) then atulee ni kiasi gani inahitajika kufanya hiyo operation ili tuweze kumchangia na kulimaliza hili tatizo for once and for all; badala ya kuendelea kuumia kila wiki kutumia kiasi hicho kikubwa cha fedha.
ReplyDeleteMungu wangu wee.
ReplyDeleteNdio kusema kwamba kila wiki anahitaji takriban milioni moja, na unasema kuwa tatizo hili laendelea kwa muda mrefu sasa.
How has she been managing?
NAAFIKI WAZO LA MCHANGIAJI WA KWANZA. SULIHISHO LA KUDUMU NI KUPATA FIGO NYINGINE TU.
ReplyDelete