Na Mohamed Hamad, Manyara
ZAIDI ya maduka kumi ya wafanya biashara wa soko kuu la kiteto Mkoani
Manyara yameteketea kwa moto ulioibuka usiku wa kuamkia leo Aug 23 mwaka huu na kusababisha hasara ambayo thamani halisi haijafahamika kwa haraka
Inasemekana kuwa moto huo ulianza saa nane ambapo chanzo chake kinadaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme katika moja ya maduka hayo ambayo yameteketea ibaya baada ya watu waliofika kushindwa kuudhibiti moto huo
Kwa mujibu wa Ofisa mtendaji wa kijiji cha Kibaya Fatuma Ngao amedai
kuwa miongoni mwa vitu vilivyoteketea ni pamoja na maduka hayo kumi
nyaraka mbalimbali za Serikali, ofisi ya kijiji pamoja na baraza la
ardhi la kata.
Alisema kuwa nyaraka hizo ni pamoja na vitabu mbalimbali ambazo
zilitumika kama kumbukumbu za Serikali, viti na meza ambazo zilitumika
katika kuihudumia jamii ya Kibaya na vitongoji vyake.
Ngao alisema alipata taarifa hizo kupitia matangazo yaliyotolewa
kwenye moja ya msikiti mkuu mjini hapo ya kuwaomba wananchi hao ili
waweze kufika kuokoa mali zilizokuwa zinateketea katika soko hilo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...