Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue Jumatano tarehe 21 Agosti 2013 jioni alitangaza Makatibu Wakuu na Manaibu Katibu Wakuu Wapya katika Press Conference iliyofanyika Ukumbi wa Ikulu Mawasiliano.

Ifuatayo ni orodha kamili ya majina na vituo vya kazi vya Makatibu Wakuu Wapya na Manaibu Katibu Wakuu, pamoja na waliohamishwa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Wahusika wana maelimu makubwa makubwa lakini wote watakua makatibu na kukaa wizarani tu basi,kuna watu wana mpaka P.h.D za kilimo lakini watakua Dar wakila upepo, wakati huohuo kauli mbiu ni kilimo kwanza.Kwakweli Tanzania profession haitendewi haki hata kidogo.

    ReplyDelete
  2. Mdau no 1, nadhani si kwamba Tz profession haitendewi haki, bali sisi watz ndo kikwazo zaidi tunazidi ubinafsi ona hata wale walioteliwa kwa kuzingatia fani zao wamefanya lipi?

    Watu hawana huruma na nchi,la kwanza mtu akiteuliwa hivyo anawaza nitafisadi wapi?

    AIBU KWAO WOTE.

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Ndugu Edwin Kiliba, hakika unastahili mana ni mchapakazi sana. Mungu akutangulie kwenye kazi zako.

    ReplyDelete
  4. Hahahahaha Wadau hapo juu!

    Ingawa Wizara ya Kilimo imehamishia Makao yake huko Temeke-veterinary, nilikuwa nashangaa sana kuona Ofisi ya Idara ya Kilimo cha Kisasa ikiwepo Jijini Darisalama pale Posta Mpya Pamba House kwa mika kibao iloyopita.

    Hivi wandugu Kilimo cha Kisasa na Jiji la Darisalama wapi na wapi?

    Kwa nini Ofisi ya mfano ya kilimo cha kisasa hicho isiwepo maeneo yanako tekelezwa Kilimo kwa vitendo huko Mabuki-Mwanza,Dakawa-Morogoro, Kibaigwa-Kiteto ama Ludewa-Iringa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...