Mkurugenzi wa Kampuni ya kizalendo ya Kotes (T) Ltd, Max Komba (wa pili kulia-waliosimama), akikagua uchimbaji mtaro kwa ajili ya kutandika nyanya za mfumo wa mawasiliano kwenye kituo cha Polisi Oysterbay, Dar es Salaam, kuunganisha kwenye mkongo wa mawasiliano wa taifa. Kulia ni Mhandisi wa masuala ya ICT, Makao Makuu ya Polisi,  Mosses Maganza na watatu ni mhandisi wa Kotes (T) Ltd, Mohamed Sibuga.  

HABARI KAMILI

JESHI la Polisi nchini limechukua hatua za kujiimarisha zaidi katika kuukabili uhalifu kisasa zaidi kwa kuamua kuviunganisha vituo vyake vikubwa kwenye mtandao wa mawasiliano katika mkongo wa taifa. 
Kufuatia hatua hiyo, ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano hayo ya kuunganishwa kwenye mkongo wa taifa wa mawasiliano, umeshaanza kwenye vituo vikubwa vya polisi katika mikoa ya Mwanza, Arusha, Kilimanjaro, Zanzibara na jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, jana, Mkurugenzi wa Kampuni ya Kotes (T) Limited iliyopewa na jeshi la polisi kutengeneza mindombinu hiyo, Max Komba, alisema, ujenzi huo ulianza kwenye Kituo cha Polisi Kurasini, Chuo Cha Polisi Chang'ombe na Oysterbay ambako ujenzi wake ulitarajiwa kukamilika jana.

Komba alisema, kampuni yake imepewa kufanya kazi katika mikoa hiyo kwa wiki tatu, tangu ilipoanza Julai 27 mwaka huu kwa mujibu wa mkataba, na ujenzi unatakiwa ume imekamilika ifikapo Agosti 20 mwaka huu.
Likizungumzia mradi huo, Jeshi la Polisi kupitia msemaji wake, lilisema, mradi huo ukikamilika utasaidia jeshi hilo kupunguza gharama na muda mwingi ambao limekuwa likilazimika kutumia katika kufuatilia kumbukumbu katika kuwatambua wahalifu.

Msemaji wa Jeshi hilo, Advera Senso, alisema, kupitia mtandao huo, vituo vilivyounganishwa vinaweza kupata taarifa na kuziona kwa wakati mmoja na kwa haraka zaidi,  jambo ambalo litawezesha kumbaini mhalifu haraka zaidi na kuwa na ushahidi wa kutosha baada ya kumnasa.

"Mradi huu ni miongoni mwa maboresho mengi tunayofanya katika jeshi la polisi ili kwenda na wakati. Hivyo baada ya kukamilisha kwenye vituo vyenye hadhi ya mikoa kipolisi, tunatarajia pia kushuka hadi ngazi za wilaya kulingana na mahitaji", alisema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. JIDOTALI Polisi!

    Ohhh mkisikia mwaka wa njaa ndio huooo unaingia, yaani itakuwa ni noma mtu unaiba huko Jangwani ama Gerezani Karikoo 'Wazee' wakiwa Msimbazi Kituoni wanakushuhudia live kwenye 'Kioo' huku Mzee Mzima IGP Mwema akiwa ameunganishwa moja kwa moja.

    Si itakuwa majoto hayo?

    ReplyDelete
  2. Mtawezaje kukabiri UHALIFU wakati ninyi wenyewe ndo wahalifu, "how is it possible" kujikabili mwenyewe, hiyo itakuwa miujiza ngoja tuone.

    ReplyDelete
  3. Kumbe Tanzania bila uhalifu inawezekana! Jamani hongereni jeshi la polisi kwa hilo, ila ingekuwa imefanyika miaka ya nyuma yani kwa sasa watu wanauawa sana na uhalifu ni mkubwa ndio wanastuka. Hivi kwa nini msijenge kimyakimya kabisa na watu wasijue kama kuna hiyo kitu ndio mngekamata weeengi mno! wangebakia kujiuliza hawa wanajuaje haya? Sasa mnapotangaza ina maana mnawaambia wahalifu wabadili mbinu za uhalifu na mnawapa alert! Tuwe kama nchi za nje. Hayo mambo yalitakiwa kuwa siri kubwa sana kwa jeshi la polisi. Ila mnafanya kazi nzuri sana na Mungu azidi kuilinda nchi yetu ya Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Ohhh huko Polisi ilipofikia hatari sio siri.

    Tuache Wizi na Rushwa, ni bora tuendeshe maisha kwa njia zingine!

    Mfano tulime hata Bustani ndogo za Michicha ktk vichochoro vya majumba yetu badala ya kuishi kwa Wizi na Mipango mipango ambayo sasa inakwenda Ukingoni,,,kama hivyo sasa mnaona Polisi ipo KIDIJITALI zaidi.

    Hivi kwa Mtaji huo wa KIDIJITALI si inakuwa ni kizaa zaa, kweli patakuwa na mahitaji ya Ushahidi au Mashahidi Mahakamani siku mtu akiburuzwa kwenye Sheria?

    ReplyDelete
  5. Hahahaha!, eee Polisi ndani ya Mtandao ?

    Mipango na Wizi sasa basi!

    Ni bora mwende Vijijini kwenu kwa Mababu na Mabibi mkajifunze Uganga wa Kienyeji!

    Kwa sasa Usajili wa Ligi ya Maisha Dirisha Dogo ''Wizi'' ili kufikia malengo ya Kimaisha linaelekea Ukingoni kufungwa.

    ReplyDelete
  6. Madalali wa Kesi Mahakamani mmeona hiyo?

    Zile biashara zenu za kutengeneza Mashahidi kwa ajili ya Kesi za Wateja wenu sasa Kwishney!!!

    Polisi itakuwa na uwezo wa kuita Taswira kwa njia ya Mtandao ili kuunasa Ushahidi moja kwa moja bila UFS yeyote ile.

    ReplyDelete
  7. Tutakula wapi Madalali wa Kesi Mahakamani?

    Hapo ni kuwa kwa Mtaji huo wa ICT Wana Usalama Polisi wametulaza njaa sana, Bundi anaunguruma nadhani ndio tumekwisha sasa!

    ReplyDelete
  8. Ahhh wapi?

    Kwani ni mara ya kwanza?, Nakumbuka Raisi wa Mareklani alipokuwa George W. Bush alipokuja Tanzania mwaka 2008 Polisi hiyo hiyo ililetewa vifaa kibao zikiwemo Kamera na yale Mabuti, na Makoti Bullet Proof wanayotumia Askari wa Pikipiki wa tiGO ,alakini cha ajabu Polisi hao hao walizihujumu Kamera zisifanye kazi ili waweze kufanya Mipango yao ya Rushwa!

    Ilikuwa Kamera zinawaumbua kwa Mabosi wao kuweza Polisi kuonekana Mitaani live wanavyopokea Mishiko.

    Kwani walifanyaje?, si wali pekenyua wakavunja system nzima!

    ReplyDelete
  9. Hii technology sio ya muujiza.. Itasaidia upashanaji taarifa tu si kwa Maana ya kuwaona wahalifu

    ReplyDelete
  10. Mie nashangaa watu wanadhania itakuwa kama ulaya no mataa! ni taarifa za simu tu hakuna zaidi ya hapo kuwa polisi ili wazipate badala ya kufuatilia huko kwenye mashirika ya simu. Jamani watanzania huwa hatuelewi kwa haraka, mdau hapo juu umesema sawa hii sio muijiza, na pia inaweza isiwe effective kama wahalifu hawatawasiliana kwa simu basi itakuwa ngumu kujua kwa njia hii! kama wale wa tindikali wanaotokea ghafla na kumwagia watu acid au pikipiki wanaouwa ghafla njiani, yani hapo ndio wanafanya wabuni njia zingine za kutowasiliana kwa simu wakipanga mikakati sasa itakuwa wao kwa wao wanapanga ana kwa ana, ndio mana nilisema wasingesema haya, nje huwa hawasemi njia gani wanafanya wangekaa kimya ikawa siri na watu wangekamatwa sana sasa wanatangaza, wahalifu watabuni njia nyinginezo! Mungu aiponye Tz, tunahitaji kuombea taifa hili sana. Juzi juzi tu wamekamata silaha zilionyeshwa na Kova,na jana nasoma mhadhiri kauwawa kwa kupigwa risasi mchana, swali je silaha ngapi ziko mikononi kwa wahalifu? wanazipataje? njia gani zinatumika kuziingiza hadi wahalifu wa chini na wa kawaida wanakuwa na silaha? Je wanaouziwa wanadhibitiwa? Je zinaletwa na nchi jirani? Je Kova atamaliza kuzikamata silaha zote? Je anajua zipo ngapi kwa wananchi wasio na uhalali wa kuwa nazo? Je ukamataji wa silaha utakuwa endelevu au ni siku ambazo watu wanauawa ndio kampeni zinafanyika? Je na tindikali watadhibiti vipi? Kweli Mungu tu aingilie kati, tunahitaji kuombea nchi ya Tz sana.

    ReplyDelete
  11. Nimecheka kweli. Hivi kumbe bado kuna watu wanaamini usanii wa polisi? Hahaahaa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...