Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akitoa taarifa ya Uchunguzi wa Matukio yaliyolalamikiwa dhidi ya askari Polisi katika Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro na Kigoma. Baadhi ya matukio hayo ni pamoja na tukio la gari la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) kutumika katika uhalifu (ubebaji bangi) katika Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, Polisi Mkoa wa Morogoro kutumia fuvu la kichwa cha binadamu kumbambikizia mfanyabiashara kwa lengo la kupata fedha na Mauaji ya mfanyabiashara wa Wilaya ya Kasulu yaliyofanywa na Askari wawili wa Jeshi la Polisi. Taarifa hiyo ameitoa katika Ukumbi wa Mikutano wa wizara hiyo, jijini Dar es Salaam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kuvua madaraka hakusaidii! Wafuiwe kazi na utumishi ili iwe fundisho! hapa mnacheza bado watatumia nafasi zao kuendeleza uhalifu tu! Asali washaionja hawa!

    ReplyDelete
  2. Ahh bwana wee, sisi tushayazoea haya, kila siku tunaambiwa panafanywa uchunguzi huu na ule mwishowe hakuna lolote linalotokea na watu wanaendelea na maisha yao kama hapajatokea lolote lile.

    Kuna kesi chungu nzima na matukio mengi tu ambayo mengine serikali ilitumia mamilioni kufanya so call uchunguzi na hakuna lolote lolote lilitendeka kuadhibu wahusika. Nani asikumbuka kesi ya yule alokua akiendesha blog ya zeutamu? kesi yake imefika wapi? serikali imetumia hela tela kumsaka na alipopatikana na kugundulika kuwa ni mtoto wa kigogo, kesi hadi leo haikutajwa.

    ReplyDelete
  3. KWANINI UWAVUE POLISI MADARAKA TU BILA KUWASHTAKI?WAVUE MADARAKA,LAKINI PIA WASHITAKIWE NAKOSA LAKUKUTWA NABANGI KAMA WANAVYOSHTAKIWA WATU WENGINE,NAHAO WENGINE WASHITAKIWE KWAKOSA LAMAUAJI,YAMSHTAKIWA,KADHALIKA NAHAO WALIOMBAMBIKIZIA FUVU MFANYABIASHARA,WASHITAKIWE NAWATOE MAELEZO HILO FUVU LABINADAMU WAMELITOAWAPI,HUENDA WAKAWA NIWAUAJI.....!!

    ReplyDelete
  4. Utani mwiingi hata ktk masuala muhimu, haya tunawasubiri kwa hamu tuwaoneshe kwamba sisi hatukua tunafuarahia.

    ReplyDelete
  5. Kwa hili mimi binafsi naona Dkt Nchimbi amefanya maamuzi magumu lakini yenye manufaa kwa jeshi lake maana maadili yalikuwa yanaporomoka kwa kasi sababu kubwa ikiwa ni tamaa ya kujipatia fedha kinyume na maadili ya kazi. Nakupongeza sana Waziri, naomba kazi hii ya kuwachunguza wanajeshi wako iendelee na hao matrafiki fake nao wachunguzwe wanatoa wapi hayo mavazi, ipo siku raia tutakataa kutii amri ya hawa matrafiki kwakutokujua yupi ni wa kweli na yupi ni fake!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...