AFANDE MWEMA FUNGA KITUO HIKI NI KERO KWETU! Kwa kweli kituo hiki cha polisi pale Ferry jijini Dar ni kero kubwa kwetu wakazi wa Kigamboni tunaovuka na magari. Unaambiwa kila saa mapolisi wake wako bize kuvuta kidogodgo cha kuingiza kibabe kwenye foleni magari ambayo hayakuwa kwenye foleni na kusababisha magari kupigana pasi na kero ya foleni isiyotembea. Kama huamini tega mtego siku moja uone kama hujanasa panya - Mdau Kigambonino...

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Ni kweli ,kuna watu wanajuana na polisi wa kituo hicho,wanachofanya ni kuzuga kama wanaegesha gari kituoni pale kama dakika kumi hivi kisha wanatokea pale na kuingia kwenye mstari.Hii huwaumiza sana wale watu wema wanaofuata utaratibu,nirahisi kuingia kwenye foleni saa 11 jioni na kuvuka saa mbili usiku kwa ajili ya watu kama hawa wenye ushirika na maasikari wa kituo hiki.

    ReplyDelete
  2. Kwa kweli ni kero kubwa kituo hiki,ukiacha wanaowaingiza kutokea kwenye parking kuna wanaowaingiza moja kwa moja utaona polisi anasimama mbele yako kukuzuia halafu anaingiza gari zake alizochukua kidogodogo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...