Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi nchini, Airtel imetajwa kuwa
moja kati ya makampuni ambayo yamekuwa yakishirikiana na serikali kwa
dhati katika harakati za kupambana na tatizo la ajali za barabarani.
Akithibitisha madai hayo, Kamanda mkuu wa kikosi cha usalama
barabarani, DCP Mohamed R. Mpinga amesema kuwa Airtel imeweza kutoa
mchango katika kupunguza wimbi la ajali za barabarani kwa kiasi
kikubwa ikitoa ushirikiano katika juhudi mbalimbali zinazofanywa na
kikosi cha usalama barabarani kwa dhumuni la kuepusha ajali za
barabarani.
"Airtel ni wadau wakubwa wa kampeni za usalama barabarani, kwa miaka
mitano mfululizo na hata mwaka huu 2013 Airtel inaendelea na udhamini
wa wiki ya nenda kwa usalama barabarani. Airtel pia imedhamini vipindi
vya elimu ya usalama barabarani katika TV - kumekucha na Jambo
Tanzania (ITV na TBC 1) na Radio one.
Pia Airtel kwa kushirikiana na Rotary club na jeshi la polisi usalama
barabarani imedhamini kampeni yenye ujumbe usemao Kuendesha + Simu =
Kifo inayowaasa waendesha vyombo vya moto kutotumia simu wakati
wakiendesha magari, vile vile mwaka jana Airtel ilidhamini mashindano
ya mpira wa miguu kwa wapanda pikipiki (Bodaboda) yaliyokuwa na lengo
la kutoa elimu ya usalama barabarani kwa waendesha pikipiki ," alisema
DCP Mpinga.
Nae Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel-Tanzania Bi Beatrice Singano
Mallya, akizungumza juu ya suala hilo, amesema "Airtel imeamua
kushirikiana na serikali katika kuhakikisha inatokomeza kabisa wimbi
la ajali za barabarani. Idadi ya vifo vinavyotokea barabarani ni kubwa
mno na ndiyo maana Airtel imeamua kujikita katika kuokoa maisha ya
wateja wake na watanzania kwa ujuma. Tunapenda kuwakumbusha watanzania
kuwa swala la kupunguza ajali za barabarani ni wajibu wa kila
mwananchi hivyo tutii sheria bila shuruti".
Airtel itaendelea kushirikiana na jeshi la polisi usalama barabarani
katika kuhakikisha lengo letu la kupunguza ajali linafanikiwa,
tumeanza kuona mafanikio na kwa kiasi Fulani ajali za barabarani
zinapungua kulinganisha na miaka iliyopita," alisema Beatrice.
Tumepatiwa Takwimua kwa na ofisi inayoratibu wiki ya nenda kwa usalama
barabarani zinabainisha ajali za barabarani zimeweza kupungua kwa
kiasi kikubwa tokea mwaka 2011 ambapo Airtel imekuwa ikishirikiana nao
katika programu mbalimbali mjini na vijijini, kabla ya hapo tokea
mwaka 1995 ajali zilikuwa zikiongezeka kila mwaka kati ya ajali 2,000
na 4,000. Lakini Mwaka 2010 ukilinganisha na 2011 ajali zilipungua
kwa 3% na 2011 na 2012 ajali zilipungua kwa 2%.
Airtel Tanzania inaendelea na kudhamini wiki hii ambapo kwa mwaka huu
imejitolea kuchapisha tena stika za usalama barabarani pamoja na
kudhamini tena mashindano ya mpira wa miguu ya waendesha bodaboda
yajulikanayo kama MPINGA CUP ambayo dhamira yake ni kuunga mkono
juhudi za baraza linaloshughulikia usalama barabarani maalum kwa kutoa
elimu kwa watumia vyombo vya moto na waenda kwa miguu barabara zote
ili kuepusha ajali.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...