WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali itahakikisha kuwa ardhi ambayo Watanzania wamepewa na Mungu haibadiliki na kuwa chanzo cha upotevu wa amani nchini.
Ametoa kauli hiyo leo mchana (Jumanne, Septemba 10, 2013) wakati akifungua mkutano wa kimataifa wa siku tatu unaojadili haki na amani katika masuala ya ardhi Tanzania ulianza jana jijini Dar es Salaam.
“Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha kuwa ardhi yetu haileti laana bali inabakia kuwa baraka ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia. Ninawasihi wale wote wenye mamlaka na utoaji wa ardhi wahakikishe kuwa wanatimiza wajibu wao wanaposimamia masuala ya ardhi ili haki isipotee na hatimaye kuepusha migogoro ya ardhi,” alisema.
“Ninawasihi Watanzania iwe ni wanasiasa, viongozi wa dini, asasi za kiraia, wasomi na umma wote kwa ujumla. Ninaomba tuitunze amani tuliyonayo na tutambue kwamba Tanzania ndiyo nchi pekee tuliyojaliwa kuwa nayo. Madhara ya ukosefu wa amani ni makubwa. Tuangalie nchi za wenzetu zenye migogoro na tuone jinsi machafuko hayo yatatuathiri sisi wenyewe, watoto wetu na wajukuu wetu,” alisisitiza.
Waheshiwa wetu swala la amani kama kweli mnalihubirini kwa moyo wekeni nguvu kwenye utawala bora na kutokomeza Rushwa kwani hata hiyo ardhi chanzo ndo hicho tunachokijua,amani haitahubirwa kwa maneno tu bila vitendo.
ReplyDelete