Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez akishangilia leo baada ya kurudi kwa kishindo kwenye ligi Kuu ya Uingereza baada ya kupiga mabao mawili wakati Bwawa la Maini likiipiga Sunderland bao 3-1 na kuruka hadi nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo.
Akicheza kwa mara ya kwanza toka April 21 kutokana na kufungiwa michezo 10 kwa kumng’ata mtu, Suarez aliona nyavu mara mbili baada ya kutengenezewa na Daniel Sturridge, ambaye alifunga bao la kwanza akiwa ndani ya sita.
Emanuele Giaccherini  alirudisha moja lakini Bwawa la maini waligangamara, na endapo kama Liva ingeshinda 2-1 wangebaki katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, lakini bao la tatu la Suarez limewanyanyua.
Suarez alirejea rasmi wiki iliyopita wakati Bwawa la Maini lilipokipiga na Man U na kufungwa kwa bahati mbaya bao 1-0, ila mchezo wa leo ulikuwa wa kwanza kwake na kaonesha yeye na Sturridge ni ‘mapacha’ wenye sumu kali uwanjani.

CHEKI MSIMAMO HADI SASA. 
MAN U MLIE TU MWAKA HUU...


1Arsenal6615
2Liverpool6413
3Tottenham6413
4Chelsea6411
5Southampton6311
6Man City6710
7Hull6-110
8Everton529
9Aston Villa619
10West Brom618
11Cardiff6-18
12Man Utd607
13Swansea6-17
14Norwich6-27
15Stoke6-27
16Newcastle5-37
17West Ham6-15
18Fulham6-54
19Crystal Palace6-63
20Sunderland6-101


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mh! Hili bwawa lako la maini naona kama ni bidhaa ya kichina, urembo mwanzo tu, wenye shughuli yao wanakuja, hawana haraka.

    ReplyDelete
  2. Table hiyo tuwekee ikifika January, nina hakika hutaiweka!!

    ReplyDelete
  3. Jamaa ndugu zangu mashabiki wa Manu siku hizi wamepoteza kauli, wakiniona tu watafuta sababu za kuondoka ati wana mashughuli. Nawaonea huruma.Ila huyo kocha mpya mwambie atafute kazi nionavyo mimi akipoteza mechi mbili hivi zaidi, atanyolewa manyoya ya shingo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...