- Sasa kuongozana na Mawaziri mguu kwa mguu
- Asema kazi yake ya kuijenga chama inahitaji watu makini kama mtu hawezi kasi yake awapishe.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikaribishwa kwa kahawa katika kijiji cha Budalabujiga wilaya ya Itilima mkoani Simiyu ambapo Katibu Mkuu alifanya ziara ya siku moja wilayani hapo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikaribishwa kwa kahawa katika kijiji cha Budalabujiga wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Katibu wa Itikadi na Uenezi ameongozana na Katibu Mkuu wa CCM katika ziara ya mkoa wa Simiyu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo wakati akikagua Bwalo la chakula la shule ya sekondari ya kata ya Kanadi, wilayani Itilima mkoa wa Simiyu.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata ya Kanadi baada ya kutembelea bwalo na bweni la shule hiyo ambapo aliwasihi wanafunzi kusoma kwa bidii na kuahidi kuwapatia sola.
Katibu Mkuu wa CCM akiwa amembeba mtoto Dhahabu katika kituo cha afya cha Nangale wilaya ya Itimila mkoani Simiyu.
Chuo kikuuu cha Bagamoyo kimeanza-ishwa lini?
ReplyDeleteWengine mapya yanatupita.
MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
Inaelekea kinana ni hatari ila kazi ya kuwatembele wanyonge iendane na kasi ya kusafisha magamba ndo kilio kikubwa
ReplyDeleteShiriki katika kuandaa Elimu na Afya, Bora na mazingira salama kwa kizazi ulichobeba. Hayo ndiyo mapenzi ya kweli kwa kizazi kizima!
ReplyDelete