Meneja wa kiwanda cha Pareto Martin Oweka kilichoko Wilayani Mufundi katika mji wa Mafinga.
========  ======  ========
KIWANDA CHA PARETO(PCT) WAPATA HASARA BILIONI 1.4

Na Denis Mlowe,Mufindi

KIWANDA cha Pareto(PCT) cha Wilayani Mufindi, mkoani Iringa kimepata hasara ya zaidi ya shilingi Bilioni 1.4 baada ya kushindwa kununua pareto kwa wakulima na kuizalisha kwa kipindi cha miezi miwili. Meneja wa kiwanda Martine Oweka alisema mpaka sasa mitambo ya kuzalishia zao hilo ilisimama kwa muda kutokana na kukosekana kwa malighafi hiyo baada ya kuwepo kwa wanunuzi wengi, ambao wamekuwa wakisafirisha nje ya nchi licha ya kuwepo kiwanda.

Alisema hasara kubwa inatokana na uwekezaji wao katika zao hilo ambapo, kwenye msimu wa kilimo walitumia Sh milioni 500, kuwanunulia wakulima miche ya pareto, elimu juu ya kilimo hicho sambamba na ujenzi wa maeneo ya kukaushia zao hilo, ili kuongeza sumu. " Mwezi Julai ilikuwa tupate tani 100 za pareto kwa wakulima lakini tuliambulia tani 20 wakati mwezi huu wa agosti kati ya tani 200 ambazo ilikuwa tukusanye, tumeambulia tani 30 tu, hii ni hasara kubwa sana kwetu hatukuwa na kibali cha kununua pareto kwa wakulima japo hiki ni kiwanda pekee Tanzania,”alisema Oweka.

Alisema kibali cha kununua zao hilo kwa wakulima ilikuwa wapatiwe mwezi juni mwishoni, lakini badala yake walipewa August 21, mwaka huu kikiwa kimechelewa kwa miezi miwili.Hata hivyo alisema hasara ya Sh Bilioni 1.4 waliyoipata kwa kushindwa kuzalisha zao hilo, inawaghalimu wakulima ambao, wengi wao wamehifadhi pareto ndani kinyume cha taratibu za zao hilo, ambalo ubora wake hutegemea ukali wa sumu.

“Mkulima akivuna Pareto halafu akahifadhi ndani kwenye unyevu kwa muda mrefu inapoteza sumu kiasi ambacho hata sisi wanunuzi inakuwa vigumu kuinunua kwani, ubora wa pareto ni kiwango cha sumu iliyopo,”alisema.Aliongeza kuwa kushindwa kununua pareto hiyo kumeisababishia hasara serikali kwa kuwa imekosa fedha za kigeni ambazo hutokana na mauzo ya nje ya zao hilo mara baada kuzalishwa kiwandani hapo. Aliwataka wakulima kutokata tamaa na badala yake waendelee kuzalisha zao hilo na kuiomba serikali kulinda soko la pareto.

Kwa upande wao wakulima, wameiomba serikali kuhakikisha kuwa zao hilo halifi na kuona namna ya kulinda viwanda vya ndani vyenye uhakika wa soko badala ya kuruhusu soko huria, wakati malighafi hiyo hata ndani ya nchi haitoshelezi mahitaji. Uwezo wa kiwanda cha Pareto cha Mafinga ni kuzalisha tani 6,000 kwa mwaka lakini badala yake, kimekuwa kikiambulia tani 2,5000 pekee.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. Bosi Martin Oweka,

    Yaani pamoja na Mahesabu yote uliyoshuka na maandishi ya mchanganuo kwenye Ubao hapo nyuma yako kwa Marker pen nyekundu na bluu bado SHIRIKA LA PARETO LINAPATA HASARA YA TShs. 1.4 BILIONI?

    ReplyDelete
  2. Mzigo wa 1.4 Bilioni,

    Ni mkubwa sana hapo Kijijini Mafinga kuliko mifuko yenu ya suruali na makoti yenu ya baridi Kijijini, hivyo kwa Upotevu wa mzigo huo:

    Wewe Bosi unayetoa taarifa hapa uwe wa kwanza kuisaidia Mamlaka ni vipi zitapatikana hizo!

    ReplyDelete
  3. Ohooo mapesa Mabilioni yanapotelea Kijijini?

    Ehhh, kwa mfumuko gani wa bei Kijijini mkaijua fedha hivyo?

    Haya masihara Bongo Tanzania ni shamba la bibi!

    ReplyDelete
  4. elieza mabulaSeptember 26, 2013

    hapa sasa ndipo anapotakiwa waziri mhusika kuonesha makali kama wenzake, mawaziri wa ujenzi na uchukuzi.viwanda hivi ni vya kulinda kwa gharama yoyote ili Tanzania tusiuze malighafi naomba waziri mkuu awe anaigilia kati mambo kama haya la sivyo tutaenedelea kuwa maskini kwa miaka mingine hamsini

    ReplyDelete
  5. Hii kasi ya Ufisadi nchini inatisha!!!

    Yaani hadi Vijijini wameamka sana siku hizi na Mabilioni wanayajua nao?

    ReplyDelete
  6. Kipindi kile cha Kambarage ilikuwa hapo Mafinga Kijijini kupata Chenji ya Shilingi 100/- ile ya Noti Nyekundu ya Simba na Mmasai ni mbinde hadi uende kwenye Duka la Tajiri mkubwa sana Kijijini ama iwe ni mwisho wa mwezi!

    Lakini kwa ajabu kabisa kwa zama hizi hapo hapo Kijijini panatokea upotevu wa Mabilioni ya Shilingi !!!

    ReplyDelete
  7. Haya Mahesabu ya Benki ya Dunia kuhusu kiwango cha Umasikini hasa Kusini mwa Bara la Afrika na Jangwa la Sahara yatakuwa sio sahihi kudai watu wanaishi chini ya DOLA MOJA KWA SIKU!

    NAWAULIZA WANATAALUMA WA KIBENKI, FEDHA NA UCHUMI, JE MAHALA WANAPOISHI CHINI YA DOLA MOJA KWA SIKU KAMA HAPO MAFINGA PANAWEZA KUPOTEA (US $ 864,197.00) Tshs. BILIONI 1.4 ?

    ReplyDelete
  8. Oh,oh,oh,

    Hapo Mafinga bakuli moja la Pombe ya kienyeji ya Ulanzi halizidi Shilingi 100/= wakati Ugali kwa maharage Gengeni haizidi Shilingi 200/= huku Laki inakuwa kama ndio Bilioni moja na leo kumepotea Shs. Bilioni 1.4,

    Sasa hiyo kwa mabadilishano ya Mafinga ya Kinyalu si itakuwa ni sawa na SHILINGI TRILIONI 140 ?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...