Mpango wa Afya wa KNCU unapeleka vijijini madaktari bingwa wa magonjwa ya watoto, kinamama na sugu. 
• Madaktari bingwa waliotajwa hapo juu wamefanya kliniki 203 na kuona wagonjwa 1887 tangu Juni 2011 mpaka juni 2013. 

• Madaktari bingwa waliotajwa hapo juu huenda kwenye vituo 20 vilivyopo kwenye Mpango wa Afya wa KNCU walau mara mbili kwa mwezi. 
• Wagonjwa wenye matatizo sugu 66 waligundulika na kupewa rufaa ya kwenda KCMC. 
• Mpango wa Afya KNCU una wanachama zaidi ya 16,000 wanaopata huduma za Afya katika vituo 20 vya Afya vilivyopo kwenye mpango huo wa Afya. 
• Mafundisho ya nadharia na vitendo kuhusu jinsi ya kutambua ishara za hatarishi za magonjwa sugu yametolewa na madaktari bingwa hao kwa wahudumu wa afya wa vituo 20. 
• Wanakijiji wenye magonjwa sugu wamepata huduma kwa gharama nafuu bila kulazimika kuja mjini kwa matibabu, hivyo kuwapunguzia gharama na usumbufu 
• Watu wengi wamegunduliwa na matatizo (yaliyokuwa hatua za awali) ambayo yalishindwa kugundulika katika zahanati. Mf. Ugonjwa wa ini, cerebral palsy etc. 
• Kwa maelezo zaidi kuhusu Mpango wa afya KNCU piga namba ya bure (kwa watumiaji wa Vodacom Tanzania) 0800 754 002
 Ukaguzi wa maboresho ya ubora wa huduma za kitabibu chini ya mpango wa huduma salama (SafeCare) katika zahanati ya Mbahe.
 Wanachama wa Mpango wa Afya wa KNCU wakipata huduma katika zahanati ya Makomu.
Mmoja ya watoto waliozaliwa na kupata huduma katika mpango wa Afya wa KNCU. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Wadau naomba mnisaidie tafsiri ya daktari bingwa kwa kingereza.

    ReplyDelete
  2. Specialist, such as pediatrician, gynecologist, physician

    ReplyDelete
  3. Hatua hii ni ya kupigiwa mfano. Hongereni sana madaktari kwa kuanzia mpangi huu ni uzalendo wa hali ya juu sana Mungu awabariki sana. Na asanteni watanzania wenzangu kwa kuitikia mpango huu, tuudumishe. Mjenga nchi ni mwananchi

    ReplyDelete
  4. there is no direct translation in English, However the equivalent of daktari bingwa in english is the same as

    a Specialist doctor as mentioned above by anon sept 14, 2013

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...