Nani atatwaa taji laMiss Universe Tanzania kwa mwaka 2013? Jibu la swali hilo litajulikana kesho (Ijumaa) wakati warembo 15 kutoka mikoa mbali mbali ya Tanzania watakapochuana kwenye ukumbi wa Makumbusho ya Taifa na jumba la Utamaduni  jijini kuanzia saa moja kamilli usiku.
Warembo hao mbali ya kuwania taji la Miss Universe Tanzania ambalo kwa sasa linashikiliwa na Winfrida Dominique, pia watawania taji la Miss Earth Tanzania na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa.
Warembo hao kwa nyakati tofauti walikuwa wakitambiana huku kila mmoja akisema atatwaa taji hilo na kuiwakilisha nchi katika mashindano ya dunia yaliyopangwa kufanyika  Novemba 9 jijini Moscow, Russia.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Communications inayoandaa mashindano hayo, Maria Sarungi alisema kuwa kila kitu kimekamilika na warembo wamepania kufanya makubwa jukwaani . Maria alisema kuwa warembo wote wana ari ya juu na kila mmoja akiwa na shauku ya kutwaa taji hilo.
“Kwa upande wetu, kila kitu kipo tayari, warembo wamejiandaa vilivyo na tumeandaa shoo bora na fupi, hivyo mashabiki wa masuala ya urembo wanatakiwa kufika mapema ili kuona nani anatwaa taji na kupata tiketi ya kuiwakilisha nchi kimataifa,” alisema Maria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...