Maafisa wanadhimu, maafisa mipango na ugavi pamoja na wahasibu wa mikoa na vikosi vya Jeshi la Polisi unaofanyika moshi, mkoani Kilimanjaro. Picha na Tamimu Adam, Jeshi la Polisi.
Wajumbe wakifuatilia mada mbalimbali
zinazowasilishwa katika mkutano unaofanyika Mkoani Moshi, Mkoani Kilimanjaro
katika Chuo cha Taaluma ya Polisi. Picha na
Tamimu Adam, Jeshi la Polisi.
Na Tamimu Adam, Jeshi la Polisi Moshi Maafisa wanadhimu wa Jeshi la Polisi wa mikoa na Vikosi mbalimbali wametakiwa kutekeleza majukumu Yao kwa uwazi na uwadilifu kwa Kushirikiana bila kujali tofauti za kimajukumu kwa lengo la kuimarisha usalama, Amani na utulivu hapa nchini.Hayo yalisemwa na Afisa Mnadhimu wa Makao Makuu ya Upelelezi wa makosa ya jinai, Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP) Brown Lekey Wakati akizungumza na maafisa watendaji wa mikoa, Vikosi pamoja na wahasibu katika mkutano mkuu unaojumuisha maafisa wanadhimu,maafisa mipango na ugavi pamoja na wahasibu wa Jeshi la polisi kinachoendelea Moshi mkoani Kilimanjaro katika Chuo cha Taaluma ya Polisi (MPA). Aliongeza kuwa ufanisi wa utendaji wa Kila mtendaji katika sehemu aliyopo utapimwa kutokana na jinsi alivyoweza kupanga mipango,kugawa na kusimamia rasilimali ili kuwezesha eneo lake kuwa salama na kutatua kero mbalimbali za kiusalama. Aidha, aliwaeleza kuwa dhana ya ushirikiano na ubia na wadau mbalimbali wa ulinzi na usalama ni mpya yenye sura ya Kimaboresho inayojikita zaidi katika usasa, weledi na Polisi Jamii na ulinzi shirikishi ambao ndio utendaji wa Jeshi la polisi katika kuimarisha usalama wa raia na Mali zao. Kwa upande wake mmoja wa watoa mada wa mkutano huo, ambaye ni mkuu wa kitengo cha maendelao ndani ya Jeshi la polisi, Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP) Sospeter Kondela aliwaeleza watendaji hao kuwa hawanabudi kupanga na kusimamia rasilimali kwa weledi kwani bila kusimamia rasilimali vizuri hakuna operesheni, doria wala misako ya kukabiliana na vitendo vya uhalifu vitakavyofanyika kwa mafanikio.vilevile aliwataka maafisa wanadhimu na maafisa mipango kuweka mabango maeneo ya polisi, kufufua mipaka pamoja na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara ili kuondoa fursa na mazingira yanayopelekea wananchi kuvamia maeneo ya polisi. |
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...